Na Sophia Kingimali
MAKAMU wa Rais Dk Phillip Mpango amezitaka nchi za Afrika kuangalia namna ya kutumia teknolojia ili kuchochea maendeleo ili kukabiliana na ukosefu wa ajira kama njia ya kuchochea uzalishaji na ukuaji wa uchumi barani humo.
Dk Mpango ametoa wito huo leo februari 7,2024 jijini Dar es salaam wakati akifungua Mkutano wa 7 wa Washirika wa Kijamii wa Afrika ulioandaliwa na chama cha waajili Tanzania (ATE)Kwa kushirikiana na shirika la la kimataifa la waajili(IOE) ambapo mkutano wa siku mbili umehudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 50 barani Afrika na ni mara ya kwanza kufanyika nchini.
Amesema kuwa ujio wa mkutano huo unapaswa kutazamwa kama fursa ya utatuzi wa ukosefu wa ajira kwa vijana nchini.
“Katika maendeleo ya teknolojia, inaweza kutarajiwa kuwa uundaji wa nafasi za kazi utaathiriwa na mifumo hivyo tunatarajia mkutano huu utakuja na mwarobaini wa upungufu mkubwa wa ajira zilizopo, hivyo tunatumaini matumizia ya teknolojia yatasaidia kutengeneza ajira mpya hasa zile zinazohitaji ujuzi wa kiufundi,” amesema. .
“Baadhi ya kazi za ubora wa chini kama vile makarani wa kuingiza data na wachapaji walihamishwa na teknolojia ya kisasa. Kwa hivyo, maoni yangu ni kwamba akili bandia inaweza pia kutafsiri kuwa fursa ya kufufua tija, mapato na ukuaji wa uchumi katika bara letu. Ujio wa AI unamaanisha kuwa serikali na sekta ya kibinafsi katika bara la Afrika inahitaji kuwapa wafanyikazi wao ujuzi wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kuwawezesha kufaa katika soko jipya la ajira”Amesema.
Makamu wa rais amesema kuwa mafunzo mapya na uingiliaji kati wa ukuzaji wa taaluma ni muhimu ili kupata wafanyakazi ambao ndio uhitaji wa soko la ajira kwa siku zijazo huku akitaka kufanyika uchambuzi kwani ni muhimu ili kubaini sekta ambazo zina uwezekano wa kuona idadi kubwa ya fursa za ajira.
“Sekta ambazo akili bandia zinaweza kuongeza ajira zenye ujuzi wa hali ya juu na eneo moja la maslahi ni sekta ya kilimo ambapo inaweza kukuza uzalishaji wa ajira na utafiti wa kilimo unaolenga kuboresha aina za mbegu zenye mavuno mengi na zinazostahimili hali ya hewa ambazo zitachochea tija zaidi za kazi za baadaye. Na nadhani haya ni maswala ambayo yanahitaji umakini wa mkutano huu, “amesema.
Akizungumza kando ya mkutano huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Suzanne Ndomba-Doran amesema mkutano huo utajikita katika masuala ya uundaji wa nafasi za ajira ambapo kutakua na mada tofauti zenye kuja na mapendekezo ambayo yatayashauri namna ya kuongeza ajira nchini.
“viongozi wa kanda waluokutana leo watajadiliana kilele cha mkutano watakuja na mchango wa hati tofauti ambazo zitakuwa msaada kwa washirika wetu wa kijamii na waajiri”Amesema.
Kwa upande wake, Roberto Suarez Santos, Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Waajiri (IOE) amesema, mkutano huo unatoa fursa ya kuunda suluhisho na mbinu za pamoja za kutatua changamoto za ajira kwa vijana ambapo swala hilo lilipelekea ukosefu wa utulivu kwa kijamii.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Saidi Wamba, amesema wao kama wadau wanatarajia kujadili namna ya kuendeleza mijadala na midahalo yenye nia ya kuboresha uhusiano kati ya chama na waajiri kwa sababu ajira inamnufaisha kila mtu akiwemo. mustakabali wa sekta ya ajira.