Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji TIC John Mnali.
………..
Na Sophia Kingimali
Ziara za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika mataifa mbalimbali nchini zimezaa matunda ambapo wawekezaji wameendelea kuingia kwa kasi nchini na kusababisha kukuza uwekezaji na kuimalisha uchumi wa nchi ambapo Kituo cha uwekezaji nchi(TIC) kimewahakikishia wawekezaji kutoka nje ya nchi na ndani kuwawekea miundombinu yote ikiwemo upatikanaji wa vibali na leseni ili waweze kufanyakazi yao kwa tija na weredi.
Akizungumza leo februari 5,2024 jijini Dar es salaam wakati akiwakaribisha wawekezaji kutoka India walikuja kuwekeza katika hospitali ya Tanzanite iliyopo mkoani Mwanza Mkurugenzi wa uhamasishaji uwekezajiJohn Mnali amesema uwekezaji huo ni matokea chanya ya hamasa ya kuvutia uwekezaji unaofanywa na serikali ya awamu ya sita.
“Haya ni matokeo ya hamasa ya uwekezaji inayofanywa na Rais wetu Dkt Samia suluhu Hassan katika nchi mbalimbali Duniani ambapo anaitangaza nchi katika sekta mbalimbali kwa uwekezaji ambao tunaona hapa hii tiba utalii ambapo wenzetu watashirikiana na hospitali ya Tanzanite kutoa huduma kwa wananchi hivyo niwahakikishie vibali vyote vitapatikana kwa wakati”amesema Mnali.
Aidha Mnali ameongeza kuwa mwaka 2024 wao kama TIC ni mwaka wa uwekezaji hivyo wataendelea kutoa hamasa kwa wawekezaji kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi ili waweze kuwekeza nchini ambapo mpaka sasa wameshafanya uhamasishaji katika nchi ya China,India na Indonesia.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa bodi hospitali ya Tanzanite Jared Awando amesema wamesaini mkataba wa ushirikiano na taasisi ya ES Health care interprises Ltd ambapo kampuni hiyo imetoa kiasi cha Dolla Milioni 500 ambayo itaenda kusaidia katika shughuli mbalimbali ikiwemo maboresho ya hospitali hiyo lakini pia ujenzi wa chuo cha mafunzo.
Amesema wanatarajia kupokea madaftari wabobezi 10 kutoka india watakaokuja kutoa huduma katika hospitali hiyo ikiwemo huduma ya macho na meno.
“Hii hela tuliyopewa tutaenda kuboresha huduma hospitali ikiwemo vifaa vizuri kwa ajili ya matibabu ya binadamu lakini pia kufungua kiwanda kwa ajili ya kutengeneza dawa za binadamu na kufungua chuo cha mafunzo”Amesema Awando.
Ameongeza kuwa mkataba huo waliosaini ni wa miaka mitatu hivyo wanatarajia kutumia vyema pesa hizo ili kuhakikisha malengo waliyoyaweka yanatimia katika muda huo.