Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo leo Februari 5, 2024 jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Wataalamu wa Umoja wa Watengeneza Vyombo vya Moto Afrika (Africa Association of Automotive Manufacturers – AAAM).
Katika kikao hicho, Prof. Mkumbo amesema kuwa Kampuni ya AAAM ni ya kuaminika na hivyo Serikali ipo tayari kushirikiana nayo ili iweze kufanya utafiti wa mazingira kuhusu ukuzaji wa vyombo vya moto nchini kwa lengo la kupata matokeo sahihi ya hatua ya awali kwa ajii ya kuunda sera kuhusu masuala ya vyombo vya moto.