Waziri wa nchi (OR) Ikulu mhe.Ali Sleiman Mrembo akifungua kongamano la wadau wa kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001 lilifanyika ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Mhe. January Yussuf Makamba akimkaribisha Waziri wa nchi (OR) Ikulu Mhe. Ali Sleiman Mrembo kufungua kongamano la wadau wa kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001 lilifanyika ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini magharibi Idrisa Kitwana Mustafa akitoa salamu za mkoa katika kongamano la wadau wa kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001 lilifanyika ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kongamano la wadau wa kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001 lilifanyika ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Katibu Mkuu wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi Dkt. Aboud Jumbe akiwasilisha mada katika kongamano la wadau wa kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001 lilifanyika ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Katibu mtendaji baraza la taifa la watu wenye ulemavu Zanzibar mhandisi Ussy Khamis Dede akichangia katika kongamano la wadau wa kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001 lilifanyika ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Katibu Tawala Mkoa wa Kusini UngujaRadhia Rashid Haroub akichangia katika kongamano la wadau wa kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001 lilifanyika ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar. (PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR)
……..
Na Sabiha Khamis Maelezo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe. Ali Suleiman Ameir (Mrembo) amesema maoni ya wadau ni muhimu katika kuunda Sera madhubuti itakayonufaisha Taifa.
“Maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Mpya ya Mambo ya Nje ni muhimu sana katika kuiletea Tanzania maendeleo katika kuimarisha uchumi.”
Akizungumza wakati akifungua kongamano la kukusanya maoni kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya Sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001, katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa ndege, amesema maoni hayo yatasaidia Serikali kunufaika na fursa za ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mataifa mengine.
Amesema Serikali inatambua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika maamuzi yanayohusu maslahi yao katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ameona umuhimu huo na kupendekeza kuwa wadau wa Serikali zote mbili wanashirikishwa katika kutoa maoni.
“Rais Samia aliielekeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kuhakikisha kuwa wadau wa Serikali zote mbili wanashirikishwa katika kutoa maoni yao mahususi kabla ya kukamilisha mchakato wa marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Nchi ” alisema Waziri Mrembo.
Alieleza kuwa kwa kuzingatia hilo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar pamoja na Taasisi ya Uongozi umeandaa kongamano hilo la tatu ikiwa ni muendelezo wa Makongamano yaliofanyika Dar es Salam na Arusha kwa lengo la kukusanya maoni ya wadau mbali mbali yatakayoweza kuleta Sera yenye tija na kukidhi matarajio ya wananchi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwa kupitia kongamano hilo washiriki watapata fursa ya kuelewa kwa kina Mambo muhimu yaliomo katika Sera ya Mambo ya Nje katika dhana ya uchumi wa Buluu na Diplomasia ya Uchumi na kuzingatia masuala mapya yaliopendekezwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kongamano hilo ambae pia ni Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Yussuf Makamba, amesema nchi zenye misingi ya utawala bora ni muhimu kuwashirikisha wadau na wananchi katika kutoa maoni kuhusu Sera ni jambo la msingi ili Sera inayotungwa iwe bora na yenye kuleta tija kwa Watanzania.
Aidha Januari Makamba amefahamisha kuwa, Marekebisho ya sera hiyo yamekuja kufuatia Mabadiliko na Maendeleo ya Dunia hivyo ni vyema kila mmoja kushiriki kwa Maendeleo ya Taifa.
Alieleza kuwa kongamano kama hilo la kukusanya maoni ya wadau kuhusu marekebisho ya Sera mpya ya Mambo ya nje ya mwaka 2001 linatarajiwa kufanyika katika Kisiwa cha Pemba tarehe 10 Februari, 2024 katika Kiwanja cha kufurahishia Watoto Tibirinzi, Chake chake.
Wakichangia mada katika kongamano hilo baadhi ya washiriki wamesema kuwa Sera hiyo izingatie mahitaji ya watu wenye ulemavu pamoja na kuwaomba itakapokamilika iletewe mrejesho kwa jamii katika hali ya maandishi ili kila mmoja aweze kuifahamu sera hiyo.
Katika kongamano hilo maada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo sera ya mambo ya nje na masula mepya yanayopendekezwa pamoja na dhana ya uchumi wa buluu kwa kuzingatia masuala mepya yanayopendekezwa.