Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara, leo Februari 5,2024 kinaendesha uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wa chama hicho.
Nafasi hiyo inayogombaniwa na Saduga Manawa Mossy akichuana vikali na Justine Nyamuru awali ilikuwa ikishikiliwa na Samweli Ghati .
Zoezi ilo la uchaguzi linasimamiwa na viongozi wa juu wa chama hicho kutoka Kanda ya Serengeti na Mkoa wa Mara.