Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) katika Semina iliyoandaliwa na Jeshi la Magereza kuhusu utendaji kazi wa Jeshi hilo, kwa ajili ya Kamati hiyo, iliyofanyika jijini Dodoma, leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vita Kawawa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Vita Kawawa (wapili kushoto), wakiwa na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Maafisa Magereza, wakitoka Gereza Kuu Isanga, baada ya kufanya ziara katika Gereza hilo, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akimkabidhi zawadi ya kikapu kilichotengenezwa na wafungwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Vita Kawawa (kushoto), baada ya kumaliza ziara katika Gereza Kuu Isanga, jijini Dodoma, leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Mzee Ramadhani Nyamka. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Vita Kawawa (katikati waliokaa), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (wapili kushoto), Kaimu Katibu Mkuu, Miriam Mmbaga (kushoto), Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Mzee Ramadhani Nyamka (wapili kulia), Naibu Kamishna wa Magereza, DCP Jeremiah Katungua (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo, baada ya kumaliza ziara katika Gereza Kuu Isanga, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Vita Kawawa (kulia) akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini baada ya Semina iliyoandaliwa na Jeshi la Magereza kwa ajili ya Kamati hiyo, iliyohusu utendaji kazi wa Jeshi, jijini Dodoma, leo. Katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Miriam Mmbaga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.