Na Sophia Kingimali
Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Mrisho Mrisho amekanusha taarifa zinazo sambaa kwenye mitandao za ucheleweshaji wa kutoa mzigo katika bandari hiyo ikiwemo mzigo wa sukari na kusema kuwa bandari hiyo inafanyakazi kwa saa 24.
Hayo yamebainishwa leo Februari 4,2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kazi zinazofanyika bandarini hapo lakini pia kutolea ufafanuzi swala la madai ya bandari kusimamisha meli iliyo beba sukari
Amesema kuwa shughuli za kutoa mzigo bandarini zinaendelea kwenye gate zote na kuna meli zinashusha mizigo masaa 24.
Amesema kuanzia Februari 1 hadi 4 zaidi ya meli kumi wamehudumia na leo kuna meli tatu zinaondoka tayari baada ya kushusha mizigo hivyo amewahakikishia watanzania bandari inafanyakazi.
“Sio kweli mzigo hautoki bandarini ili utoke mtu lazima awe amekamilisha taratibu zote na ndani kwani bandarini kuna taasisi 30 zinafanyakazi aseme taasisi gani imkwamisha mzigo usitoke na bandari ya Dar es Salaam ni baba inatupiwa mzigo shughuli bandarini zinaendelea,”amesema Mrisho.
Aidha ameongeza kuwa taarifa zinazo sambaa kuwa bandari ya Dar es Salaam wanakwamisha sukari sii za kweli kwani wao walipokea barua ya ombi kutoka Bodi ya Sukari wafanyie kazi kuna meli tatu zenye sukari ziweze kutoka haraka.
“Tumepokea ombi hili sisi bandari tumepokea tumefanyia kazi kwa sababu ni mahitaji muhimu mzigo wa sukari unahitajika sokoni sisi tumetekeleza jukumu hili mengine ni aulizwe Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari,” ameeleza.
Aidha amesema kuwa pamoja na changamoto za muvua za El-Nino wamehudumia zaidi ya meli 86.
Sambamba na hayo Mrisho amesema kipindi cha nyuma kwa mwezi walikuwa wanahudumia tani milioni 1. 6 kwa sasa wanahudumia tani milioni 2.5 kwa mwezi wanahitaji kuvuka zaidi.