Wakazi wa Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro wameiomba Serikali kuona namna ya kuwasaidia, kuwahamisha wananchi waliyopo kwenye mkondo wa daraja la mradi wa SGR, kuondokana na adha ya mafuriko ambayo katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikijitokeza kila mwaka
Wameyasema hayo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz M. Abood alipofika kutoa pole kwa waadhirika wa Mafuriko katika Kata za Lukobe na Kihonda ambapo alifika mtaa wa Azimio eneo lenye waathirika wengi.
Wakazi hao walipata nafasi kuzungumza na kutoa maoni pamoja na kero mbele ya mbunge ambapo wamesema awali kabla ya Mradi wa reli ya Mwendo kasi maeneo hayo hayakuwahi kupata mafuriko tofauti na sasa baada ya kujengwa tuta ambalo linazuia maji kupita kwenye njia yake na kurudi kwa wananchi
Rashidi Kibwana mmoja wa wakazi wa Azimio pamoja na kuiomba Serikali kuwatatulia changamoto inayowakabili pia ameishukuru Serikali ya Mhe Rais Samia kwa namna ambavyo imekuwa karibu sana na wananchi wake pale wanapopatwa na changamoto.
Pia amemshukuru Mbunge Mhe Abood kwa namna ambavyo kila wakati bila kujali muda wala nyakati amekuwa kimbilio na sikio la wananchi katika Jimbo lake la Morogoro Mjini.
‘Mimi nimeishi Morogoro sasa zaidi ya miaka 48 lakini sijawahi kuona Mbunge anayependa wananchi na kuwasaidia bila kuchoka kama alivyo Mhe Abood” Alisema Rashidi
Baada ya kusikiliza kero hizo ikamlazimu kuwaita wataalamu wanaosimamia na kujenga mradi wa SGR kwa Morogoro.
Baada ya kusikiliza kero na maoni ya wananchin Mhe Abood ametaka kuwa watulivu wakati Serikali ikitafakari namna ya kuwasidia na kuwahakikishia wakazi wa Kata za Lukobe na Kihonda kuwa kilio chao Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekisikia na anakitafutia ufumbuzi.
Pia Mhe Abood akawaomba wasimamizi wa amradi wa SGR kutumia athari za mvua kuangalia kwa namna gani wataweza kuzuia maji yasiingie kwenye makazi ya watu.