Wamesema mkoa wa Njombe upo juu kijiografia hivyo imekuwa sababu kubwa ya kuwa na watu wenye kimo kifupi huku wengine wakisema asili ya wakazi wa Njombe ni wafupi wa kurithi.
”Tunaomba watalaamu waliofanya utafiti huu warudi wakanye tena utafiti kwa kutozingatia kiashiria cha ukondefu na uzito kwasababu watu wa Njombe wengi wanaufupi wa asili lakini akili wanazo,alisema Nyagawa diwani Wanging’ombe”
Aidha madiwani hawa wameshauri jitihada za mapambano dhidi ya udumavu kuongezwa zaidi katika kutoa elimu katika jamii hususani wanawake na akina mama ambao ndiyo wana jukumu kubwa la malezi huku pia wakitaka taasisi za elimu na vituo vya kliniki kupewa kipaumbele.
Awali mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Claudia Kitta wakati akiwasilisha ujumbe wa serikali amewataka madiwani kutumia nafasi zao kutoa elimu kwa wananchi juu ya lishe na udumavu ili kutokomeza janga hilo.
Katika hatua nyingine Kitta amewataka viongozi wa serikali na chama cha mapinduzi wilayani Humo kujiandaa na mapokezi ya katibu wa siasa ,Uenezi na Mafunzo ndugu Paul Makonda anaetarajiwa kupokewa katika kijiji cha Halali februari 8 akitokea Jijini Mbeya.
Katika baraza hilo pia Tanesco,Tarura na Ruwasa zimetupiwa lawama kwa kushindwa kutoa huduma za ipasavyo kwa wananchi jambo ambalo limemsukuma Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe Dr Peter Nyanja DED Wanging’ombe kuliahidi baraza hilo kukutana na taasisi hizo ili kujua kwa kina juu ya utekelezaji wao huku pia akisema halmashauri inakuja na sheria itakayozuia magari yenye uzito mkubwa kuingia mashambani kubeba malighafi ili zisiharibike.
Suala la lishe amesema halmashauri hiyo imekusudia kutokomeza kabisa tatizo hilo kwa kuja na mpango madhubuti wa elimu kwa jamii.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe Onesmo Lyandala ametumia baraza hilo kusisitiza utekelezaji wa mpango wa kutokomeza udumavu kwa kuzingatia zaidi siku 1000 za unyonyeshaji ambao umeanzishwa na mkuu wa mkoa wa Njombe ili kuwa kizazi bora siku za mbeleni na kisha kulitaka shirika la umeme Tanesco kueleza kwanini wilaya hiyo imekuwa na mgao wa umeme uliyopindukia.