…………………….
Manispaa ya Ubungo Mkoani Dar es salaam imetenga bajeti kiasi cha shilingi Bilioni 1.8 ambazo zitagaiwa kila Kata kwa ajili ya utekelezaji wa miundombinu ya barabara kutokana na uharibifu uliotokea kwa sababu ya mvua zinazoendelea kunyesha Ili kuondoa adha ya usafiri.
Hayo yamebainishwa leo katika kikao cha baraza la Madiwani ambacho kimeongozwa na Juma Japhary Nyaigesha ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo katika ukumbi wa Manispaa.
Akizungumza wakati akijibu hoja za wajumbe wa Baraza Hilo,Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Elias R Ntiruhungwa amewataka Watendaji Kata kuainisha barabara zenye changamoto na kutoa kipaumbele kwa barabara zinazohitaji utatuzi wa haraka wa kurekebisha.
Aidha amesema Ntiruhungwa amesema kwa mwaka wa fedha ujao Manispaa hiyo itapanga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vitendea hususani kompyuta mpakato’laptop’ kwa watendaji wa Kata wa Manispaa hiyo ili kurahisisha utendaji kazi wao na kuwezesha utunzaji wa siri wa nyaraka za Serikali.
Kwa upande wake Mhe. Juma Japhary Nyaigesha Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo amewataka Watendaji Kata hao kuendelea kushirikiana vyema na Madiwani sambamba na utekelezaji bora wa majukumu yao.
Hata hivyo Baraza la Kata la Manispaa ya Ubungo limeisisitiza Manispaa hiyo kuweka mpango madhubuti wa urekebishaji wa miundombinu ya barabara ambayo imeharibika nyakati za mvua ili kurahisisha hali ya usafiri na usafirishaji.