Wizara ya Katiba na Sheria yamshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuimariaha mifumo ya utoaji hali nchini kwa vitendo kwa kuwezesha kupata vifaa vya Tehama kwajili ya Taasisi zinazoshughulikia masuala ya Haki Jinai.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Pindi Chana kwenye hafla hiyo ya utoaji wa vifaa vya Tehama.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri Pindi Chana amesema amesema jukumu la wizara ni kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati bila kujali dinj, umbali au hali yoyote ya mtu na hili kufanikisha hilo ndio maana ziara inaendelea kusimamia uwekaji wa mifumo na miundombinh ya TEHAMA thabiti ya kuhakikisna wananchi wote wanafikiwa na huduma za kisheria ikiwemo kupaga elimu ya masuala ya sheria, ufunguaji wa kesi, uendeshaji wa kesi, upatikanaji wa nyaraka za kesi na ushahidi, hukumu na maamuzi ya kesi na uwepo wa vyombo vya utoaji haki katika ngazi za kijamii na upatikanaji wa hudjma za msaada wa kisheria.
Waziri Pindi Chana amesisitiza kuwa Wizara inatambua umuhimu wa Taasisi za haki jinai katika majukumu waliyodhaminiwa ya utoani wa huduma za kisheria na upatikanaji haki nchini.
“Haki ndiyo kila kitu kwani haki huliinua Taifa mbele ya Mwenyezi Mungu” Alisema Waziri Pindi Chana.
Pia, Waziri Pindi Chana amesema kuwa serikali imejizatiti katika kuimarisha masuala ya utoaji na upatikanaji haki nchini.
Katika kuweza kufikia lengo la upatikanaji haki kwa wakati, Waziri Pindi Chana amebainisha kuwa Serikali imeendelea kuratibu na kufuatilia uwepo wa mifumo mizuri ya kisheria ambayo itarahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati ambayo itawezesha wananchi kusogezewa huduma za kisheria popote walipo kwa gharama nafuu katika kuifikia haki.
Waziri Pindi Chana ameendelea kusisitiza kuwa “Uwepo wa mifumo, ya TEHAMA na matumizi ya Teknolojia utawapunguzia wananchi muda na gharama za kushughulikia masuala ya kisheria na badala yake watajikita zaidi katika shughuli za kiuchumi na kimaendeleo, hivyo basi kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na kuchangia katika pato la Taifa kwa ujumla.”
“Ni matumani yangu kuwa vifaa hivi vitatumika ipasavyo katika kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wananchi. Matumizi sahihi ya TEHAMA yatawezesha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi wetu ikiwemo kuwapunguzia gharama za kufuata huduma. Hii itachochea uchumi wa nchi yetu kwa kuzingatia wananchi watatumia muda mwingi katika kufanya shughuli za kuwaletea maendeleo.” Alisema Waziri Pindi Chana.
“Wizara itaendelea kushirikiana na Taasisi zote ili kuhakikisha tunaboresha maeneo yote yenye uhitaji. Lengo ni kutimiza adhma ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kufanya maboresho makubwa kwenye mfumo wa Haki Jinai nchini na eneo kubwa ni kuimarisha mifumo na miundombinu ya TEHAMA kwenye Sekta ya utoaji Haki nchini.” Alisema Waziri Pindi Chana.