Katibu Tawala Wilaya ya Ubungo Hassan Mkwawa akiongoza kikao cha Baraza la Biashara katika Wilaya hiyo ambacho kimefanyika Leo Jan,30,2024.Afisa Biashara wa Manispaa ya Ubungo Mary Mwakyosi akizungumza katika Kikao cha Baraza la Biashara akieleza kuhusu kuhusu urasimishaji wa Shughuli za Biashara ambacho kimefanyika Leo Jan,30,2024.Afisa Mkuu msimamizi wa Kodi akitolea ufafanuzi masuala ya kikodi katika kikao cha Baraza la Biashara katika Wilaya ya Ubungo ambacho kimefanyika Leo Jan,30,2024.Afisa Afya Manispaa ya Ubungo Bonifas Katikiro akizungumza katika Kikao cha Baraza la Biashara Wilaya ya Ubungo ambacho kimefanyika Leo Jan,30,2024.Baadhi ya wafanyabiashara na wadau kutoka taasisi mbalimbali wakiwemo Maafisa wa usalama walioshiriki katika Kikao cha Baraza la Biashara Wilaya ya Ubungo ambacho kimefanyika Leo Jan,30,2024.(picha zote na Mussa Khalid)
……………,…..
NA MUSSA KHALID
Wafanyabiashara wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam wametakiwa kuwa mabalozi wazuri katika suala la utekelezaji wa urasimishaji wa Biashara zao ikiwa ni pamoja na kulipa kodi kwa wakati kli kusaidia kuongea mapato katika Wilaya hiyo.
Hayo yamejiri Leo jijini Dar es salaam katika kikao cha Baraza la Biashara katika Wilaya ya Ubungo ambacho kimewakutanisha wafanyabiashara na Maafisa kutoka katika taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.
Akizungumza katika Kikao hicho Katibu Tawala Wilaya ya Ubungo Hassan Mkwawa ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wafanyabiashara kuhakikisha kwa pamoja wanashirikia na sekta binafsi lakini pia na Manispaa ili kufanya biashara zao kwa ufanisi bila ya kuwa na changamoto yeyote.
Kwa upande wake Afisa Biashara wa Wilaya ya Ubungo Mary Mwakyosi akielezea kuhusu urasimishaji wa Shughuli za Biashara amesema kuwa wameendela na zoezi la kurasimisha Biashara katika maeneo mbalimbali kwenye Manispaa hiyo ambapo Mpaka sasa pia wamefanikiwa kutoa Elimu katika kata 10 kuhusu kurasimisha Biashara zao sambamba na kujiunga na mfumo wa Tausi.
Kwa upande wao baadhi ya wadau wa Biashara katika Manispaa hiyo wameeleza masuala yatakayoimarisha Maendeleo ya Uchumi Wilaya kuwa ni pamoja an Manispaa kuhakikisha inazitatua changamoto mbalimbali kwenye maeneo yao ikiwemo suala la maji,pamoja na umeme.
Hata hivyo Afisa Biashara wa Manispaa hiyo amewasisitiza wafanyabiashara kujiwekea mazoea ya kufuatilia taarifa zinazotolewa Ili waweze kujiongezea ujuzi na kipato katika Biashara wanazozifanya.