Na Sophia Kingimali.
Taasisi ya Utulivu Space inatarajia kufanya tamasha kubwa liitwalo Utulivu Experience lenye lengo la kuhusherekea Utaifa wa mtanzania kufuatia amani na utulivu uliopo nchini.
Akizungumza leo januari 30,2024 Rais wa taasisi hiyo Ibrahim Rwegerera amesema wameamua kuja na tamasha hilo lengo kuwakutanisha watu mbalimbali waliochangia kuwapo wa amani na utulivu uliopo nchini.
Amesema tamasha hilo litakua la kwanza kufanyika katika mazingira ya kitulivu ambapo litawakutanisha watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu ambao wanaasili ya kitanzania watakaa na kujadilina na kunywa chai pamoja.
“Tamasha hili linawahusu watu wote wenye asili ya kitanzania tunawakaribisha wote wacheza mpira,wasanii,wanasiasa na kila mwenye asili ya kitanzania maana hii itakua ni siku yetu ya kusheherekea Utanzania wetu hivyo tujitokeze kwa wingi hii itakua tamasha la kihistoria”Amesema
Amesema Tamasha hilo litafanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza linatarajiwa kufanyika mwezi Aprili 20,2024 katika ukumbi wa Super dom Masaki na awamu ya pili litafanyika Zanzibar mwishoni mwa mwezi novemba 2024.
Kwa upande wake mmoja wa waandaaji wa tamasha hilo Anthony Luvanda amesema tamasha hilo linatoa fursa kwa wageni kuja kujifunza asili ya mtanzania ikiwemo ukarimu na utamaduni wa Mtanzania.
“Nitoe wito kwa watu wa mataifa yote kuja kujifunza asili yetu lugha yetu,mavazi yetu ukalimu na utulivu wetu waje wajifunze utamaduni wa kiswahili”amesema Luvanda.
Aidha Luvanda amesema kuwa utulivu unaanzia kwa mtu binafsi lakini unachochewa na amani iliyopo katika nchi.
Tamasha la Utulivu Experience litafanyika Aprili 20,jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Super dom Masaki na litapambwa na wasanii wakiwemo wazamani na watu waliochangia Amani na utulivu uliopo nchini.