Kutokana na uhaba wa Sukari uliopo chini katika kipindi cha hivi karibuni Serikali imelazimika kuagiza sukari Tani 100,000 kutoka nje ili kuondoa changamoto iliyopo.
Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde ambaye ni mmoja ya wajumbe wa kamati ya bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara, kilimo na Ufugaji akiwa kwenye kiwanda cha kuzalisha sukari Sukari Mkulazi wilayani Kilosa.
Naibu Waziri Silinde amesema mpaka sasa Meli iliyobeba sukari hiyo imefika bandarini tayari kwa kushusha mzigo na kwamba sukari hiyo itauzwa kwa bei elekezi
Aidha Kampuni hodhi ya Mkulazi iliyopo Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro nayo hivi karibuni inatarajia kuingiza sokoni sukari takribani tani 500 ambazo zitakuja kupunguza makali ya uhaba uliopo sasa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Deo Mwanyika amesema kuwa, changamoto ya sukari imeanzia shambani ambapo mashamba mengi yamejaa maji hivyo kupelekea ugumu katika uvunaji