Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia), akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) katika Semina iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili yao kuhusu Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, iliyofanyika Bungeni, jijini Dodoma, leo Januari 29, 2024. Kushoto meza kuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vita Kawawa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Vita Kawawa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), Naibu Waziri, Jumanne Sagini (Watatu kushoto), Katibu Mkuu, Kaspar Mmuya (Wanne kushoto) na viongozi mbalimbali wa Wizara na Wajumbe wa Kamati hiyo, wakati wa Semina kuhusu Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, iliyoandaliwa na Wizara na ilifanyika Bungeni, jijini Dodoma, leo Januari 29, 2024. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Sehemu ya Mafunzo Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ACP Ahmad Mwendadi akiwasilisha mada kuhusu Usafirishaji Haramu wa Binadamu na Madhara yake, katika Semina iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) iliyoandaliwa na Wizara kwa Kamati hiyo nakufanyika Bungeni, jijini Dodoma, leo Januari 29, 2024. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Alexander Lupilya akiwasilisha mada kuhusu Jitihada zilizochukuliwa na Serikali katika Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Bungeni, jijini Dodoma, leo Januari 29, 2024. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji haramu wa Binadamu ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) katika Semina iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili yao kuhusu Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, iliyofanyika Bungeni, jijini Dodoma, leo Januari 29, 2024. Kushoto meza kuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vita Kawawa, Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), Naibu Waziri Jumanne Sagini (watatu kulia), Katibu Mkuu Kaspar Mmuya (wapili kulia). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.