WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Mhe. Dkt.Stergomena Tax akipanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Makao Makuu ya JKT Wilayani Chamwino Dodoma leo Januari 29,2024.
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Mhe. Dkt.Stergomena Tax ,akimwangilizia maji mti alioupanda wakati wa zoezi la upandaji miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Makao Makuu ya JKT Wilayani Chamwino Dodoma leo Januari 29,2024.
NAIBU Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis,akipanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika leo Januari 29,2024 katika Makao Makuu ya JKT Wilayani Chamwino Dodoma .
Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akipanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika leo Januari 29,2024 katika Makao Makuu ya JKT Wilayani Chamwino Dodoma .
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Mhe. Dkt.Stergomena Tax,akizungumza mara baada ya kuongoza zoezi la upandaji miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika leo Januari 29,2024 katika Makao Makuu ya JKT Wilayani Chamwino Dodoma.
NAIBU Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis,,akizungumza mara baada ya kupanda miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika leo Januari 29,2024 katika Makao Makuu ya JKT Wilayani Chamwino Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule ,akizungumza mara baada ya kupanda miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika leo Januari 29,2024 katika Makao Makuu ya JKT Wilayani Chamwino Dodoma.
Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akielezea mikakati ya JKT katika kuendelea kupanda miti kwenye kambi zote za JKT kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Januari 29,2024 .
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Mhe. Dkt.Stergomena Tax,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuongoza zoezi la upandaji miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Makao Makuu ya JKT Wilayani Chamwino Dodoma leo Januari 29,2024.
Na.Alex Sonna-CHAMWINO
KATIKA kuelekea kilele cha Maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 60 Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Mhe. Dkt. Stergomena Tax amewaongoza JKT katika zoezi upandaji miti Makao Makuu ya JKT Wilayani Chamwino Dodoma huku akielezea umuhimu wa kufanya tathmini ya idadi ya miti iliyopandwa hapo awali.
Akizungumza leo Januari 29,2024 mara baada ya kushiriki zoezi hilo Waziri Dkt Stergomena Tax amesema kuna miti mingi inapandwa kupitia kampeni mbalimbali lakini matokeo hayalingani na zoezi linalofanyika..
Amesema kuwa sehemu nyingi miti inapandwa lakini inatelekezwa na inakauka na tunatumia rasiliamali nyingi na inapotea ni vyema uwekwe utaratibu wa usimamizi wa miti inayopandwa ili matokeo yaweze kuonekana.
“Tunapoanza Kampeni mpya ya kupanda miti katika msimu mpya ni vyema tukatathmini miti iliyopandwa msimu iliopita ili kujua udhaifu kupitia kampeni iliyopita ili kurekebisha kupitia kampeni mpya” amesema Waziri Dkt Stergomena
Hata hivyo amepongeza zoezi hilo na kusema Jeshi litakuwa mstari wa mbele katika kutunza mazingira kwa kupanda miti na kutoa rai kuhakikisha jamii inaona umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuacha kukata miti onyo na kupanda miti.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ameipongeza JKT kwa kuona umuhimu wa kupanda miti ili kulinda mazingira na kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.
“Nawapongeza sana JKT kwa kuanza kutumia nishati mbadala ya kupikia katika makambi yenu mbalimbali ili kutunza mazingira na kutoa witoa kwa kuendelea na kampeni ya kupanda miti nchini”amesema Mhe.Hamza
Awali Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema kuwa JKT itaendelea kushiriki kwa vitendo zoezi la kupanda miti katika makambi yote ya JKT ili kulinda mazingira.
“Zoezi hili linaloendelea hapa linafanyika katika vikosi vyote vya JKT na tunalichukulia kwa uzito lengo ni kuhakikisha tunapanda miti ya kutosha ili kulinda mazingira yetu na kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi” amesema.
Amesema kwa mwaka 2023 JKT ilipanda miti zaidi ya elfu 75800 imepandwa katika maeneo mbalimbali na kwa mwaka huu tumepanga kupanda miti zaidi ya 100000 katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Hata hivyo ameeleza Pia kuwa JKT imeanza kutii agizo la Serikali la taasisi zenye watu zaidi ya laki moja kuacha kutumia nishati ya kuni na mkaa kwa kuanza kutumia nishati mbadala kwa kuacha kutumia kuni lengo likiwa ni kutunza mazingira huku wakiendelea kupanda miti.