NA
KVIS BLOG/KHALFAN SAID, MNAZI MMOJA
WANACHAMA
wengi wa PSSSF waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Wiki ya
Sheria kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, wamefurahishwa na huduma
ya PSSSF Kiganjani Mobile App.
Huduma
ya PSSSF Kiganjani Mobile App, inamuwezesha mwanachama kupata taarifa zote
zinazohusiana na uanachama wake akiwa mahali popote kupitia simu yake ya
kiganjani, Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta wa Mfuko huo Bw.Gideon Mwashihongo
amesema leo Januari 28, 2024, wakati akitoa elimu ya matumizi ya huduma
mtandao.
Bw.
Kizza Sostenes, Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba, Wilaya ya Temeke,
ameupongeza Mfuko huo kwa kutoa huduma zake kidijitali.
“Nimefaidika
sana baada ya kufika hapa, nimeelekezwa jinsi ya kutumia huduma ya PSSSF
Kiganjani na nimeijaribu ni huduma nzuri na rahisi kutumia.” Amesema Bw.
Sostenes.
Mwanachama
mwingine Bi. Lightness G. Msuya, yeye amesema huduma ya PSSSF Kiganjani Mobile
App, inasaidia kuokoa muda, kwani yeye kama mtumishi, inamsaidia kupata taarifa
za Mfuko akiwa mahali popote.
Kwangu
mimi huduma hii inanipunguzia gharama za usafiri kufuata huduma kwenye ofisi
za PSSSF, kuanzia sasa silazimiki kwenda PSSSF, baada ya kujiunga kwenye huduma hii, kwani
simu yangu inatosha.” Amesema Mwnachama mwingine wa PSSSF, Bw. Kudura Said
Kondo, mtumishi wa Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
ushiriki wa Mfuko kwenye maonesho hayo, Bw. Kikula Suleiman, kutoka Kurugenzi ya
Huduma za Sheria PSSSF Makao Makuu amesema, PSSSF kama taasisi iliyoundwa
kisheria ni mdau mkubwa wa Mahakama na watumishi wa mahakama na taasisi
nyingine za umma ni wanachama wa Mfuko huo, hivyo ushiriki wa Mfuko kwenye
Maonesho ni fursa nzuri ya kutoa huduma na elimu kwa wanachama.
“Katika
jitihada za kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora na rafiki tumeamua
kujikita kutoa elimu ya huduma za PSSSF kiganjani Mobile App, PSSSF ulipo
Mtandaoni Member Portal.” Amesema na kuongeza, kwa kutumia huduma hiyo
tunaamini inatoa uhuru sio tu kwa wanachama lakini pia kwa waajiri kuweza
kulipia michango na kujihudumia wenyewe, yaani self-service.” Amefafanua Bw. Suleiman.
Maonesho
hayo ya siku saba yaliyobeba kauli mbiu “Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa
Taifa: Nafasi ya Mahakama na Wadau katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki
Jinai” yamezinduliwa rasmi Januari 27 2024, na yatafikia kilele Januari 30, 2024.
Mtaalamu
wa Mifumo ya Kompyuta Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Gideon Mwashihongo (katikati), akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile
App, kwa wanachama wa PSSSF waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho
ya Wiki ya Sheria viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kupitia
PSSSF Kiganjani mwanachama anaweza kupata huduma zote zitolewazo na Mfuko bila kulazimika kufika ofisi za PSSS
Bw.
Kikula Suleiman (aliyesimama), kutoka Kurugenzi ya Huduma za Sheria PSSSF Makao
Makuu, akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile App, kwenye banda la Ofisi
ya Taifa ya Mwendesha Mashtaka Kanda ya Dar es Salaam kwenye maonesho ya Wiki ya
Sheria, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Januari 28, 2024.
Mtaalamu
wa Mifumo ya Kompyuta Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Gideon Mwashihongo (kulia), akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile
App, kwa mwanachama wa PSSSF, Bi. Lihhtness G. Msuya, kwenye banda la PSSSF, Januari 28, 2024.
Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Gideon Mwashihongo (kulia), akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile App, kwa mwanachama wa PSSSF, Bw. Kudura Said Kondo kwenye banda la PSSSF, Januari 28, 2024.
Bw.
Kizza Sostenes (kulia), Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba, Wilaya ya
Temeke, akihudumiwa na Bi. Hellen Mollel, Afisa Mafao PSSSF.