Na Sophia Kingimali.
Katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Taasisi ya Mtetezi wa mama mkoa wa Dar es salaam imempongeza kwa kuimarisha demokrasi nchini ikiwa ni pamoja na kulinda amani na kuinua uchumi wa Taifa.
Akizungumza na waandishi wa Habari januari 27,2024 mwenyekiti wa Taasisi hiyo mkoa Mohammed Chande amesema wanaendelea kumuunga mkono Rais katika yote aliyoyafanya na anayoendelea kuyafanya katika taifa kwani yamekua chachu kubwa ya maendeleo ya Taifa na ya mtu mmoja mmoja.
Amesema katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais wamefanya mambo mbalimbali ya kijamii kama kufanya usafi,kutembelea wagonjwa,kufanya mazoezi kwa kukimbia lakini pia michezo mbalimbali kama mpira wa miguu na mpira wa pete.
“Katika kuendelea kusapoti juhudi za mama katika siku yake hii muhimu ya kuzaliwa leo tumefanya mazoezi lakini pia tumetoa huduma za afya bure na kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama mjamzito na watoto”Amesema Chande.
Aidha ameongeza kuwa Rais ameonyesha kwa vitendo ukomavu wa kidemokrasi kwa kuruhusu maandamano yaliyofanywa na CHADEMA na kuwahakikishia wanapata ulinzi na kuzuia fujo.
“Mama yetu Dkt Samia amefanya mambo makubwa sana katika nchi anapaswa kupongezwa sana kwani kuna mambo ameyafanya hayakuweza kufanyika tangu kuubwa kwa nchi hii hatupaswi kukaa kimya hata wapinzani wenyew wameona wameandamana kwa amani wameenda wanapokusudia wamepita kwenye barabara nzuri wamepewa ulinzi nchi imebaki na utulivu na amani haya yote ni matunda ya Rais Dkt Samia”Amesema Chande.
Kwa upande wake mwenyekiti wa hamasa mkoa wa Dar es salaam Renfred Chavaro amesema Rais amekua mfano mkubwa kwa nchi kwa kuleta maridhio katika vyama vya siasa lakini pia katika sekta nyingine.
Amesema kulikuwa na migogoro mingi kipindi cha miaka ya nyuma inatotokana na vyama vya siasa hivyo Rais kwa kuleta 4R kumepelekea nchi kuwa na amani na vyama vya siasa kukaa meza moja na kujadiliana.
“Kwa mambo makubwa ambayo Rais wetu ameyafanya yanatufanya kuwa kipaumbele kumsemea na ndio maana tunasema ukimvaa tunakuvaa kwa hoja mama anatosha hakuna mfano wake”Amesema Chavaro