Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda Watumishi wa serikali katika sekta ya afya, wauguzi ama madaktari watakaobainika kupelekea kifo kwa wagongojwa kwasababu ya uzembe wao wa kuchelewa kutoa huduma yapaswa wachukuliwe hatua kali zaidi na isiihie tu kuwasimamisha ama kuwabadilisha vituo kwani tabia hiyo inaweza kuhamishiwa huko wanapohamishiwa.
Mwenezi Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kahama Mkoani Shinyamga ambapo alipokea kero kutoka kwa akina mama ya kutopewa huduma bora kutoka hospitali ya kahama na wakati mwengine kuombwa hongo.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Ndugu. Mboni Mhita amemthibitishia Mwenezi Makonda kuwa Serikali ngazi ya Wilaya tayari imewasimamisha kazi baadhi ya wauguzi na madaktari katika hospitali hiyo ikiwa ni sambamba na kumuondoa DMO wa Wilaya ya Kahama, Pia wanaendelea kuhakikisha watumishi wanaokiuka maadili wanachukuliwa hatua mara moja.