Mtumishi wa Mungu Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi akimkabidhi kadi ya gari Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Chang’ombe Aram G. Mkangale katika Ibada iliyofanyika leo Januari 28, 2024 Buza Kwalulenge, Wilaya ya Temeke, Jijini Dar es Salaam.
Mtumishi wa Mungu Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi akizungumza jambo katika Ibada iliyofanyika leo Januari 28, 2024 Buza Kwalulenge iliyokwenda pamoja na kukabidhi Gari kwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Chang’ombe.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Chang’ombe Aram G. Mkangale akizungumza jambo katika Ibada iliyofanyika leo Januari 28, 2024 Buza Kwalulenge iliyokwenda pamoja na kukabidhiwa Gari na Mtumishi wa Mungu Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi.
Baadhi ya waumini wa Mtumishi wa Mungu Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi wakiwa katika Ibada.
Picha ya gari ambalo Mtumishi wa Mungu Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi ametoa Zawadi kwa Jeshi la Polisi Wilaya wa Chang’ombe kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa shughuli za Jeshi.
………..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mtumishi wa Mungu Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi ametoa Zawadi ya Gari kwa Jeshi la Polisi lenye thamani ya shillingi milioni 40 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa shughuli mbalimbali jambo ambalo litasaidia kuongeza ufanisi katika kudhibiti vitendo vya uhalifu.
Akizungumza leo Januari 28, 2024 Jijini Dar es Salaam katika Ibada iliyokwenda pamoja na kukabidhi Gari kwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Chang’ombe, Mtumishi wa Mungu Nabii Domonic Kiboko ya Wachawi, amesema kuwa lengo ni kulisaidia Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu katika kutoa huduma kwa jamii.
Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi amesema kuwa viongozi wa serikali wanapaswa kupewa ushirikiano pamoja na kutii mamlaka katika kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikiwa.
“Tutaendelea kusimama na serikali kuanzia ngazi ya mtaa kwa kufanya kazi kwa ukaribu, lengo ni kuisaidia jamii” amesema Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi.
Amesisitiza umuhimu wa umuhimu wa kuwa na moyo wa kujitoa kwa ajili ya shughuli za kijamii jambo ambalo litaleta tija kwa Taifa.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Chang’ombe Aram G. Mkangale amemshukuru Mtumishi wa Mungu Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi kwa kutoa zawadi ya gari kwa ajili matumizi ya shughuli za kijamii.
Mkangale amesema kuwa gari hilo litatumika kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakazi wa Kata ya Buza katika kuwafatilia wahalifu na kudhibiti vitendo ambavyo sio rafiki.
“Nampongeza Nabii Kiboko ya Wachawi kwa kutupatia gari, Kanisa lina wajibu wa kutoa malezi bora kwa waumini ili waweze kuishi maisha ya ustarabu kupitia mafundisho ya neno la Mungu” amesema
Amesisitiza umuhimu wa kutoa malenzi na mafundisho ya neno la Mungu ambayo ni rafiki katika maisha yetu ili kuweza kuwa wastarabu katika maisha.
“Kanisa linaweza kuisaidia huduma za kijamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo kutoa elimu, huduma za afya, Mchungaji Dominic Kiboko ya Wachawi ametimiza uwajibu wa kutokomeza uhalifu” amesema.