Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa akizungumzia vitu vilivyokamatwa ndani ya msako wa wiki moja
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa akionesha vitu vilivyokamatwa ndani ya msako wa wiki moja
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
……………………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linaendelea kufanya msako dhidi ya watu wanaojihusisha na matukio ya kihalifu ili kuwaepusha wakazi wa Mkoa huo na wimbi la uhalifu unaoweza kusababisha hofu itakayowafanya washindwe kufanya shughuli mbalimbali za kujipatia kipato kwa amani.
Hayo yamebainishwa Jana Ijumaa Januari 26, 2024 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa wakati akitoa taarifa ya kuanzishwa kwa msako Maalum kwaajili ya kudhibiti na kuzuia matukio ya kihalifu katika Mkoa huo kwa waandishi wa habari.
Ameeleza kuwa taarifa kuhusu uhalifu na wahalifu zimeendelea kupatikana kutokana na ukusanyaji wa taarifa fiche zinazohusu wahalifu ambayo ni kazi inayofanywa kwa weledi na Askari wao.
“Taarifa nyingine tumeendelea kuzipata kutoka kwa wananchi wasiopenda uhalifu na kupitia ushirikishwaji mkubwa wa jamii unaofaNaofanywa na Jeshi la Polisi kupitia mikutano kati yetu na wananchi inayoendelea kufanyika katika Kata mbalimbali ambapo tumepata mafanikio makubwa katika kuwafichua wahalifu kwenye mitaa mbalimbali”, Amesema Kamanda Mutafungwa
Amesema katika msako wa wiki moja walioufanya wamefanikiwa kuwatia mbaloni washukiwa mbalimbali wa matukio ya kihalifu wakiwemo watuhumiwa wa kujihusisha na vitendo vya uhalifu 47,kuingia nchini bila kibali 5, watuhumiwa wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya 51,watuhumiwa wa mauaji 13 na watuhumiwa wa kuvunja nyumba na kuiba 17.
Aidha, amesema kuwa jumla ya watuhumiwa 335 wamekamatwa ambapo watuhumiwa 133 wamehojiwa na kufikishwa mahakamani na watuhumiwa 202 bado wanaendelea kuhojiwa na Upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
“Miongoni mwa vielelezo vilivyokamatwa katika msako huo ni simu za aina mbalimbali zaidi ya 50,dawa za kulevya aina ya mirungi,misokoto ya bangi,vifaa vya kufanyia uhalifu pamoja na mali zilizoibiwa sehemu mbalimbali katika makazi ya watu.