Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) akimkabidhi Zawadi ya Cheti cha Sifa (Certificate of Merit) Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo katika hafla ya maadhimisha siku ya forodha duniani yaliofanyika leo Januari 26, 2024 katika Hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata akizungumza jambo katika hafla ya maadhimisha siku ya forodha duniani yaliofanyika leo Januari 26, 2024 katika Hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) akimkabidhi Zawadi ya Cheti cha Sifa (Certificate of Merit) mdau wa Forodha Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro katika hafla ya maadhimisha siku ya forodha duniani yaliofanyika leo Januari 26, 2024 katika Hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna wa Forodha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA,) Bw. Juma Hassan akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya maadhimisha siku ya forodha duniani yaliofanyika leo Januari 26, 2024 katika Hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Wadau wa forodha kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata.
……….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeadhimisha siku ya forodha duniani kwa kutoa zawadi ya Cheti cha Sifa (Certificate of Merit) kwa wadau ambao wametoa mchango mkubwa katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu kwa ufanisi, huku wakiaidi kuendelea kuboresha mifumo ili utekelezaji wa majukumu yao yasiwe kikwanza cha biashara.
TRA imetoa Cheti cha Sifa (Certificate of Merit) kwa vyombo vya habari, Jeshi la Polisi Kanda Maalamu ya Dar es Salaam, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Benki ya NMB na CRDB, Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI) pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).
Akizungumza leo Januari 27, 2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya utoaji vyeti kwa wadau, Kaimu Kamishna wa Forodha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA,) Bw. Juma Hassan, amesema kuwa siku ya forodha duniani (International Customs Day) imelenga kuwajulisha umma kuhusu shughuli zinazofanywa na forodha.
Bw. Hassan amesema kuwa kupitia siku hiyo wameweza kuwatambua wadau wa forodha ambao wamefanya kazi zao kwa ufanisi na kuleta tija kwa Taifa.
“Tunasimamia maeneo mengi, hivyo peke yetu hatuwezi kutokana na shughuli nyingi ikiwemo kusimamia uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi” amesema.
Amesema kuwa wametoa zawadi kwa wadau wachache kwa ajili ya kuwawakilisha wengine kwani wapo wengi wanaoshirikiana nao katika kutekeleza majukumu.
Amesema kuwa jukumu la msingi la forodha ni kuraisisha biashara, pamoja na kuhakikisha watu wanafata taratibu wakati wa kuingiza au kutoa bidhaa ikiwemo ukusanyaji wa kodi.
“Tumeweka mikakati katika kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa ufanisi kwa kuboresha mifumo, kuongeza ushirikiano na taasisi ambazo tunafanya nazo kazi” amesema.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkuu wa Dar es Salaam Albert Chalamila, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amempongeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa vitendo.
Mpogolo ametoa shukrani kwa wadau wa forodha nchini kwa kufanya kazi kubwa ambayo imeleta maendeleo kwa wananchi, huku akisisiza muhimu kwa kujenga uzalendo na heshima kwa wafanyakazi wa TRA katika utekelezaji wa majukumu.
Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya forodha duniani “Kuwatambua washirika wa Forodha, wa zamani na wapya, ambao watawezesha kutimiza malengo ya Forodha”