…………………..
NA MUSSA KHALID
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Hashim Komba anatarajiwa kuanza ziara ya mtaa kwa mtaa kuipeleka serikali karibu na wananchi katika kufanya utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye maeneo yao.
Hayo ameyaeleza leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maendeleo ya ubungo sambamba na mafanikio katika miaka mitatu ya Rais Samia Suluh Hassan.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa ndani ya miaka mitatu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya afya wamepokea fedha Bilioni mbili na Milioni mianane ambazo zimesaidia katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Kimara Baruti sambamba na uwekaji wa vifaa wa kisasa na madaktari ambao wameendelea kutoa huduma kwa wananchi.
‘Rais ameendelea kutulete fedha za ujenzi wa kituo cha afya ambapo tumejengewa Kituo cha Afya Kwembe,Amani,Goba kwa Mill 500,Makuburi kwa Mill 500,Zahanati Msingwa na Temboni ili kuwarahisishia wananchi huduma za Afya kwa karibu’amesema Komba
Aidha akizungumzia sekta ya Elimu,DC Komba amesema wamepokea fedha zaidi ya Bill nne na Milioni Miamoja ambapo wamejenga shule mpya ya kisasa na kubwa ambayo imeshapokea wanafunzi wa kidato cha tano wanaongia kidato cha sita ambayo imekusanya watoto wa kike wanaoandaliwa kuwa wanansayansi wa baadae kwa ajili ya manufaa ya nchi.
Mkuu wa Wilaya Komba amesema kuwa kwenye elimu sekondari wamepokea fedha za ujenzi wa shule za kisasa ikiwemo King’azi Sekondari Kata ya Kwembe Mill 528,pia wamejengewa shule ya kisasa eneo la Ubungo Nationa Housing.
Pia amesema serikali imeipatia Wilaya hiyo fedha Bill 1 kwa ajili ya kujenga shule mpya na madarasa ya sekondari katika kata ya Goba eneo la Muungano na hivi karibuni watakwenda kumtangaza mkandarasi wa mradi huo.
Vilevile katika suala la miundombinu ya Barabara DC Komba amesema kuwa kazi kubwa imeendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali hasa ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi zote wanazifanyia maboresho na kuzijenga.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amezungumzia miundombinu ya soko,ambapo amesema wameendelea kuimarisha Masoko yaliyopo kwenye Manispaa hiyo ili kuweza kuongeza mapato kwa serikali.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kuendelea kuonyesha ushirikiano kwa viongozi ili kuweza kufanikisha kwa wakati miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye Wilaya hiyo.