Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Januari 25, 2024 amemsindikiza na kumuaga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar Es Salaam mara baada ya kumaliza Ziara yake nchini Tanzania.
Rais Salvador alikuwa nchini kwa Ziara ya Siku Tatu, pamoja na maeneo mengine alitembekea katika kiwanda cha ‘Tanzania Biotech Products ltd’ (TBPL) na kuzungumza na wafanyakazi ambapo alisisitiza jukumu muhimu la TBPL katika jitihada za kutokomeza Malaria nchini.
Ziara za Viongozi wa Kimataifa kuja Tanzania ni fursa ambazo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuzifungua kwa lengo la kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Mataifa mengine Duniani ili kuleta maendeleo nchini.