Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza wakati wa kufungua kikao cha kazi cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita Rafiki vya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Makatibu Wakuu hao ambao wamekutana Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS), iliyopo Kibaha, mkoani Pwani, leo Alhamis Januari 25, 2024, kujadili masuala mbalimbali, ni kutoka vyama vya SWAPO (Namibia), ZANU-PF (Zimbabwe), ANC (Afrika Kusini), MPLA (Angola) na FRELIMO (Msumbiji).
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akitoa hotuba ya ufunguzi, kufungua kikao cha kazi cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, ambao wanakutana katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJLNS), Kibaha, mkoani Pwani. Pamoja na Komredi Nchimbi, viongozi wengine waliokutana katika kikao hicho kujadili agenda mbalimbali ni pamoja na Komredi Sophia Shaningwa, Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO cha Namibia, Komredi Obert Moses Mpofu, Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU- PF cha Zimbabwe, Komredi Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha ANC cha Afrika Kusini, Komredi Francisco Mucanheia, ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO cha Msumbiji, Komredi Manuel Domingos Augusto, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA nchini Angola (wa pili kushoto) na (mwenye suti nyeusi) (picha na Scolastica Msewa).
Makatibu Wakuu wa Vyama Sita Marafiki vya Ukombozi Kusini mwa Kusini, wakiwa katika picha ya pamoja, wakati walipokutana kwa ajili ya kikao cha kazi, kujadili agenda mbalimbali katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS) iliyopo Kibaha, mkoani Pwani. Kutoka kulia ni Komredi Obert Moses Mpofu, Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU- PF (Zimbabwe), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa CCM (mwenye shati ya kijani), Komredi Sophia Shaningwa Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia), Komredi Francisco Mucanheia ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO (Msumbiji), Komredi Manuel Domingos Augusto, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa MPLA (Angola) na mwishoni kushoto ni Komredi Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini)
………………………..
VICTOR MASANGU KIBAHA