Na Sophia Kingimali
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Idara ya Forodha inatarajia kuadhimisha siku ya forodha Duniani ambapo kitaifa yatafanyika Jijini Dar es salaam lengo likiwa kufikisha ujumbe kwa umma juu ya shughuli zinazofanywa na forodha nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo januari 24,2024 jijini Dar es salaam Kaimu Kamishna wa Forodha TRA Hassan Juma amesema wamekuwa wakifanya kazi na wadau mbalimbali wakiwemo serikali,makampuni binafsi na umma.
“Sisi mwaka huu 2024 tutaadhimisha siku hii hapa jijini Dar es salaam lengo letu ni kufikisha ujembe kwa umma lakini pia kutambua wadau ambao tunashirikiana nao katika kufanya shughuli za forodha”amesema Juma.
Ameasema kitengo cha forodha wanajukumu la kutoa takwimu sahihi za bidhaa zinazoingia nchini lakini pia inajukumu kubwa la kusimamia mapato ya serikali ambapo idara hiyo inakusanya asilimia 40 ya mapato yote yanayokusanywa na TRA.
“Tunajukumu la kusimamia mipaka yote ambayo watu na bidhaa zinazoruhusiwa kuingia na kutoka nchini kwani umoja wa forodha Duniani moja ya mpango wake mkubwa ni kuzuia bidhaa kupitia eneo lolote la mipaka”amesema.
Ameongeza kuwa umoja wa forodha unajukumu la kusimamia mipaka na kulinda jamii lakini pia kukagua bidhaa zinazoingia nchini na kuzimamia mpaka kupata vibali au ruhusa.
Akizungumzia namna teknolojia ilivyoweza kusaidia Kaimu Kamisha wa Forodha amesema kuwa zamani walikuwa wakiwasilisha nyaraka kwa mkono kwa sasa hicho kitu ni historia kwani nyaraka zinatumwa kwa mtandao, ambapo unapata tathmini ya kila kitu hapo hapo pamoja na Kulipa.
Pia ukaguzi wa Mizigo amesema kuwa wanatumia kifaa maalumu cha ukaguzi ambacho hufanya kazi kwa muda mfupi zaidi ambapo zamani ilichukua muda mwingi na rasilimali watu wengi zaidi.