CHADEMA waunga mkono zoezi hilo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Januari 24, 2024 ameongoza mamia ya Wananchi wa Mkoa kufanya usafi eneo la Mbezi Malambamawili Jijini humo
Akiongea baada ya kufanya usafi RC Chalamila amesema kufanya usafi ni kudhibiti magonjwa ya milipuko ambayo hivi karibuni yamekua yakiripotiwa katika baadhi ya mikoa kama kipindupindu, vilevile kufanya usafi ni Kupendezesha Jiji letu hivyo kila mmoja ashiriki kufanya usafi katika eneo lake iwe ni tabia.
Aidha RC Chalamila ametoa ufafanuzi wa upotoshaji katika mitandao juu Usafi na maandamano ya CHADEMA hakuna uhusiano wowote, “Tanzania ni moja CCM ni Tanzania, CHADEMA ni Tanzania usafi hauna itikadi za Chama chochote, muda wa siasa chafu umepita na wakati tushindane kwa hoja” Alisema RC Chalamila
Vilevile Mhe Mkuu wa Mkoa ametoa rai kila mmoja kuilinda Dar es Salaam kutokana na umuhimu wake kwa Taifa na Wananchi kwa Ujumla, lazima kutambua Mkoa huu ndio kitovu cha Biashara, pia ni center ya diplomasia vilevile ndio taswira ya Nchi alisistiza Mhe Chalamila
Sambamba na hilo RC Chalamila amewashukuru CHADEMA kwa ushiriki wao katika zoezi la usafi kwa kuwa usafi sio Siasa ambapo amepokea ombi la mmoja wa wanachama wa CHADEMA ndg James Oyaro kuomba eneo la soko Kimara, pia Mhe Mkuu wa Mkoa amesema wafanyabishara wa Mbezi mwisho waendelee na biashara anachoitaji kuona ni usafi na ubunifu ambao hauathiri watu wengine.
Vilevile RC Chalamila amepokea vifaa vya usafi kutoka kwa wadau wa usafi Benki ya CRDB, NMB, DAWASA na TCC na kuzikabidhi Wilaya ya Ubungo ambapo ametoa shukrani kwa wadau na kutoa rai kwa wadau wengine kuunga mkono kampeni ya Usafi katika mkoa huo
Mwisho Mhe Mkuu wa Mkoa katika zoezi hilo aliambatana na Viongozi wengine akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi Rehema Madenge, Katibu wa CCM Mkoa Ndg Adam ngalawa Viongozi wengine wa CCM Mkoa na Wilaya ya Ubungo, Viongozi wa Taasisi, Benki pamoja na Watumishi.