*Waacheni watoa taarifa waandamane, Sisi tuendelee kuchapa kazi kuwatumikia ninyi Watanzania.
……….
Kati ya sifa kubwa za Mkoa wa Manyara ni shughuli za Kilimo na Ufugaji kama njia ya kuingiza kipato na kukuza Uchumi.
Shughuli hizo zote ili kufikia malengo makubwa zinahitaji msaada wa usimamizi, uboreshwaji na uwezeshwaji ambao kiini kikubwa cha kufanya hivo ni serikali yetu ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Samia ni mwenye dhamira ya dhati katika kufanikisha hayo kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM lakini yawezekana wapo baadhi ya wasaidizi wake kutofanya kazi yao vema na hoa ndio ambao Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda atawafichua na hatua kuchukulia dhidi yao kuhakikisha Imani ya Watanzania wengi kwa CCM inaendelea kusimama imara na kuongezeka.
Leo ndio leo, asemaye kesho muongo, Waacheni watoa taarifa waandamane, sisi tuendelee kuchapa kazi.