Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amepewa uchifu wa Wamasai rasmi alipopokelewa mkoani Arusha leo tarehe 23 Januari, 2024.
Makonda amepewa uchifu huo alipokutana na kuzungumza na Baraza la Wazee wa Mkoa wa Arusha pamoja na Viongozi wa Dini.
Vilevile amevalishwa vazi kama ishara ya Kijana jasiri na shupavu.
Baraza hilo la Wazee limempa Baraka ya kuendelea kuwa na nguvh ya kulitumikiabTaiga katika kumsaidia kazi Mwenyekiti CCM Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akzingumza na Wazee na Viongozi wa Dini, Makonda ametanguliza salamu za upendo na shukrani kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Ndugu. Emanuel Nchimbi.
Huu ni muendeleo wa Ziara yake ya Mikoa 20 Back To Back.