Waziri wa Ujenzi Ndugu. Innocent Bashungwa amemthibitishia Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Nsugu. Paul Makonda ya kwamba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi tayari imeshampata mkandarasi na kabla ya tarehe 25 februari, 2024 mkataba wa kuanza ujenzi utasainiwa na kazi kuanza ambapo amemueleza kuwa kama iwapo mkandarasi akaenda kinyume na utaratibu basi bondi yake itatumika kama fidia.
Waziri Bashungwa amesema barabara hiyo itakuwa na urefu wa kilomita 100 na itapelekea kufungua uchumi na mawasiliano ya watu wa Same na maeneo mengine ya jirani ambapo amesema yote ni dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Makonda alimpigia simu Waziri Bashungwa na kumtaka kutolea majibu ya barabara hiyo mara baada ya kupokea changamoto hiyo kutoka kwa Wananchi hao wa Same akiwa mkoani kilimanjaro kwa muendelezo wa ziara yake.