– Azitaja Barabara na Madaraja ambayo yaliharibiwa na mvua na kusema Wakandarasi wapo kazini
– Asema Dar es Salaam haijamezwa na mvua
– Awataka waliojenga mabondeni kuhama Mara moja
-Apiga marufuku Shughuli za kibinadamu kando kando ya Mito
-Tarehe 23- 24 zoezi kubwa la Usafi litaendelea
-Asisitiza wazazi kuwapeleka watoto shule
– Kuhusu taarifa ya vifo vya maji asema Kama vipo au havipo taarifa itatolewa na Mamlaka husika
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo Januari 22, 2024 amewahakikishia wana-Dar es Salaam kuwa Miundombinu ya msingi yote iliyoharibiwa na mvua itarudishwa kwenye Mahali pake haraka iwezekanavyo
RC Chalamila ameyasema hayo katika Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Ofisi yake iliyopo Ilala Boma Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa huyo amezitaja barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua kuwa ni pamoja na Barabara ya Mtongani Kunduchi, Daraja la Mbweni JKT, Daraja la Mbopo, Daraja la Goba, Daraja la Makulunza, Daraja la Kivule, Daraja la Msumi, ambapo amesema wakandarasi tayari wapo kazini kuhakikisha huduma zinapatikana kwa haraka
Hata hivyo RC Chalamila amesema kuwa Dar es Salaam iko salama, HAIJAMEZWA na yaliyotokea ni ya kawaida ambapo Serikali ya Mkoa inaendelea kuyaratibu
Kuhusu waliojenga mabondeni Mkuu huyo wa Mkoa amewataka kuhama Mara moja kwani wanahatarisha maisha yao na pia madhara ya kuendelea kuishi huko ni makubwa Sana
Vile vile RC Chalamila amewapiga marufuku wote wanaofanya Shughuli za kibinadamu kando kando ya Mito na kusema baadhi ya barabara zilizovunjika au kusombwa kifusi chake ni kutokana na Shughuli za kibinadamu
Aidhaa, Mhe. Chalamila amesisitiza kuwa Kampeni kubwa ya Usafi ya tarehe 23-24 Januari, 2024 itaendelea Kama lilivyopangwa na si kampeni ya kisiasa hivyo isihusishwe na kuzuia maandamano ambapo vyombo vya dola vitafanya Usafi kwenye maeneo yao na maeneo ya barabara watafanya Usafi makandarasi, vikundi mbalimbali na wadau wengine wote lengo ni kuzuia magonjwa ikiwemo kipindupindu
Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa wazazi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kuwapeleka watoto wao shuleni na marufuku walimu kudai michango kwa watoto hao
Mwisho kabisa RC Chalamila ameelezea kuwa taarifa za vifo vya maji Kama zipo au hazipo anayepaswa kutoa taarifa hizo ni Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wataalamu wa Afya baada ya kufanya postmoterm ili kubaini