Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM)Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amezungumza kuhusu katibu wa NEC Itikadi, Mafunzo na Uenezi CCM Paul Makonda kutokuwepo katika hafla ya mapokezi ya katibu mkuu huyo makao makao makuu ya CCM Dodoma
Dkt. Nchimbi amesema kuwa amesikia baadhi ya watu wakizungumza kutokuwepo kwa Makonda katika Hafla hiyo
Dkt. Nchimbi amesema kuwa anatambua kutokuwepo kwake Ndugu makonda katika hafla hiyo kutokana na kuumpa kibali cha ruhusa ya kuendelea na kazi ya kukinadi chama mikoani hivyo wananchi wajue kuwa hajatoroka
“Mwenezi yupo hajatoroka nimempa kibali yupo mikoani anafanya kazi”Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Aidha Dkt. Nchimbi amewataka wanachama wa chama hicho kukitetea chama kuanzia nyumbani mpaka kwenye mitandao ya kijamii