Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amemwagiza Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Geofrey Mkinga kuanza kazi mara moja ,usiku na mchana kurudisha mawasiliano ya miundombinu ya barabara zote zilizoharibika ili kuwezesha shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea kama awali.
Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff ameagiza kukarabatiwa haraka daraja la Tanganyika, Mbopo, Msumi na Goba Majengo yaliyopo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Madaraja hayo yameharibiwa na mvua kubwa iliyonyesha tarehe 20 January,2024 na kusababisha uharibufu mkubwa na kukata mawasiliano.