Na Sophia Kingimali
Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka viongozi wa chama hicho kufanyakazi kwa karibu na watendaji wa serikali kwa weredi na si kwa kiburi.
Hayo ameyasema leo januari 20,2024 wakati akipokelewa rasmi Jijini Dar es Salaam tangu alipoteuliwa kwenye nafasi hiyo.
Amesema chama hakipaswi kukwepa wajibu wake wa kuisimamia serikali lakini kinapaswa kusimami kwa kufuata weredi.
“Chama cha mapinduzi kitaendelea kutimiza ahadi zake na kuisimamia serikali na naahidi kushirikiana na viongozi wenzangu kukiimarisha chama lakini pia kuhakikisha hatumuangushi Rais wetu”Amesema.
Akizungumzia maandamano amesema wananchi na wanaCCM wanapaswa kuyapuuza maandamano hayo kwani hayana tija kwa taifa.
Amesema kukimbilia kwenye maandamano ni dalili ya uoga kwani uongozi thabiti unapimwa kwa kutekelezaji na hoja.
“Kukimbilia kwenye maandano ni dalili ya uoga na kushindwa niwasihi wana CCM na wananchi kwa ujumla wanapoona maandamano yao wajue wameshindwa kufikiri kupitia ubongo wao sasa wanafikiri kupitia miguu yao”Dkt Nchimbi Katibu mkuu CCM.
Aidha ametoa rai kwa vyama vya siasa kuendelea kushirukiana na CCM ipo tayar kushirikiana na chama chochote cha siasa na milango ya ofisi yake ipo wazi.
Amesema viongozi hao wasiasa na wana CCM wanapaswa kuyaeleza mazuri yaliyofanywa na serikali bila aibu.
“Hakuna sababu ya chama kutopata ushindi katika uchaguzi wa serikali ya mitaa na uchaguzi mkuu 2025″amesema
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Abas Mtevu amesema chama kinatarajia kushinda kwa kishindo mitaa yote 574 ya mkoa wa huo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema wanatekeleza kwa vitendo ilani ya chama hiko hivyo viongozi wanapoanza kampeni hawatapata tabu kujieleza kwa wananchi badala yake kazi zinajieleza zenyewe”
“Tunatekeleza ilani vizuri ili chama kisipate tabu na hata mvua zilizonyeesha leo tunawaahidi wananchi kesho miundombinu yote iliyoleta shida leo kesho itakuwa sawa”amesema Chalamila.