Na Sophia Kingimali
Wamiliki wa maroli nchini(TATOA) wameishukuru serikali kwa kuwezesha kupatikana kwa fidia kwa maroli 22 yaliyoungua moto nchini Kongo mwaka 2014.
Akizungumza na waandishi wa habari leo januari 18,2024 jijini Dar es salaam mwenyekiti wa TATOA Elias Lukumay amesema upatikanaji wa fidia hizo umetokana na juhudi ya serikali nchini kushirikiana na serikali ya Kongo.
Amesema kumekuwa na ucheleweshwaji mkubwa wa fidia pindi majanga yanapotokea nje ya mipaka ya Tanzania hivyo ametoa rai kwa taasisi za bima kuhakikisha wanashughulikia changamoto hiyo haraka ili pindi yanapotokea majanga fidia ipatikane kwa wakati.
“Kumekuwa na ucheleweshwaji mkubwa wa fidia pindi matatizo yanapotokea nje ya mipaka yetu nafikiri kwa hili kwa taasisi za bima kama NIC mnakitu cha kujifunza ili muweze kuboresha huduma zenu”Lukumay
Kwa upande wake mkurugenzi wa masoko na mahusiano NIC Karimu Meshack ametoa rai kwa wananchi kukata bima zenye uhakika na kutunza nyaraka muhimu ili pindi yanapotekea majanga waweze kufidiwa kwa wakati.
Amesemo moja ya changamoto iliyochelewesha fidia kwa waathiri wa magari hayo ni ukosefu wa kopi za nyaraka zilizoungua lakini pia Ajali kutokea nje ya mipaka ya Tanzania.
“Kwa bima yetu ya NIC mtu akipata madhara anafidiwa kwa muda wa siku saba tu akiwa ndani ya nchi na nyaraka zake zote muhimu na tunampango wa kuboresha zaidi ikiwezekana fidia itoke ndani ya saa 24″amesema
Sambamba na hayo amewataka wananchi kuacha kutumia vishoka kwenye ukataji wa bima kwani unamadhara makubwa pindi yanapotokea majanga.
Nao waathirika wa ajali hiyo ambao pia ni mnufaika wa fidia hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti wameishukuru serikali na TATOA kwa kuwasaidia kupata fidia zao pia wametoa rai kwa wa miliki wa maroli kufuata sheria zote katika biasahara ili waweze kusaidika pindi yanapotokea madhara kama hayo.
Ajali hiyo ilitokea nchini Kongo mwaka 2014 kwenye maegesho ya magari ambapo magari zaidi ya 100 yaliungua ambapo 36 kati yao yalikua ya wanachama wa TATOA ambao wapo waliopata malipo ya moja kwa moja na leo wamewafidia 22.