Kamishna mkuu wa Chama cha ADC
David Msuya Barozi wa vijana na watoto wanaopinga ukatili.
………………
Na Sophia Kingimali
Barozi wa vijana na watoto wanaopinga ukatili David Msuya ameiomba serikali kuzuia maandamano yanayotarajiwa kufanyika januari 24 yaliyoandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
Akizungumza leo januari 19,2024 jijini Dar es salaam Msuya amesema maandamano hayo yanataswira ya uvunjifu wa amani na kukwamisha maisha na shughuli za kijamii na maendeleo ya watu.
“Mimi niiombe serikali yetu tulivu izuie haya maandamano kwani yanampango ya kuharibu tunu yetu ya taifa wao kama wana hoja wakae mezani na kujadili na si kuhamasisha fujo itakayogharimu maisha ya watu”amesema Msuya.
Amesema endapo maandamano hayo yatafanyika yatasababisha madhara na kukwamisha huduma muhimu ikiwa ni pamoja watoto kushindwa kwenda shule,wagonjwa kukosa huduma mama lishe na wajasiliamali kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Aidha Msuya ametoa rai kwa vijana kutokubali kutumika na badala yake waendelee na shughuli zao za kujitafutia ridhiki zao kwa maendeleo yao binafsi na nchi.
Amesema CHADEMA wanapaswa kujenga hoja kwa majadiliano,kwa maandishi au kwa kutumia vyombo vya habari ili kufikisha malalamiko yao lakini si kwa njia ya maandamano.
Kwa upande wake Jumanne Sizya mkazi wa ilala amesema kama vijana wanapaswa kujikita kwenye shughuli za kijamii ili kujiletea maendeleo na kuepuka kutumika na wanasiasa katika uvunjifu wa amani.
Amesema serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha vijana na kuwainua kiuchumi hivyo ni vyema kuiunga mkono serikali na si kukubali kutumika na wanasiasa ili kuharibu amani na utulivu wa nchi.
Nae Madaraka Mfaume mjasiliamali na msanii wa maigizo nchini amesema wanaoitisha maandamano wanapaswa kujitafakari na kuangalia athari zinazotokana na maandamano kwa wanawake,wazee,walemavu na watoto.
Kwa upande wake kamishna mkuu wa chama cha ADC Doni Mnyamani amesema maandano ni haki ya kikatiba lakini matokeo yanayotokana na maandano yanaathari kubwa kwa taifa hivyo ni vyema CHADEMA wakatafakari kabla ya kufanya maandamano hayo.
Amesema haoni haja ya kuwa na maandano kwa sasa kwani madai yote ya msingi ambayo wananchi hasa wanasiasa walikuwa wanayoyahitaji yamesikilizwa.
“Mimi sioni haja ya hayo maandamano yao kwani sasa hivi nchi ipo shwari na Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan ametupa uhuru sana hivyo tunapaswa kuutumia vyema uhuru huo”amesema Doni.
Amesema viongozi wengi wanaohasisha maandamano hawakai mbele kwenye maandamano hayo badala yake wanatangulizwa wengine na madhara yanapotokea wanaumia na hatimae kubaki na ulemavu wa kudumu huku wengine wakipoteza maisha.