Na Ahmed Mahmoud
Maadhimisho ya miaka 44 ya Siku ya Posta Afrika yamekuja na maboresho ya huduma za Maduka Mtandao kwa kuanza na uboreshaji wa huduma za miamala kutuma na kupokea kwa Njia ya simu za mkononi sanjari na kuuza bidhaa.
Akiongea katika siku hiyo(Posta Day)iliyofanyika kwenye makao Makuu ya Posta Afrika Jijini Arusha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Celestine Kakele amesema Serikali kupitia Shirika la Posta wanaendelea kuboresha kwenda na Dunia katika Teknolojia ya Tehama.
Alisema lakini sio kweli kama huduma hizo zitakuwa zimepitwa na wakati ila ni sisi tutakuwa tumeshindwa kuwekeza kwa Kasi Sasa hii ni nafasi ya kuendelea kumshukuru RAIS wetu kwa maelekezo yake na maono ndio maana Shirika limeendelea kuwekeza katika matumizi ya Teknolojia ya utoaji wa huduma za kisasa hasa kuwezesha biashara Mtandao.
Alisema Shirika la Posta nchini halijabakia nyuma hivyo msingi Mkubwa ni maono ya Mh.Rais Samia Suluhu Hassan ya kuligeuza Shirika hilo kuendana na ulimwengu wa Teknolojia ya kisasa ndio maana wanakuja na biashara Mtandao kwa kinyago kinachouzwa kwa mtalii nchini kukipata Hadi nyumbani kwake Ulaya badala ya kusafiri na mizigo.
“Dunia imegeuka sana huu sio wakati wa kusafirisha barua tena ni wakati wa huduma za biashara mtandaoni nasi tunaelekea huko kama serikali na Shirika la Posta kulifanyia mageuzi makubwa kuwa na App ya Shirika ili kutengeneza faida”
Awali Mgeni Rasmi wa Siku ya Posta Waziri wa Tehama,Posta na Uchukuzi wa Zimbabwe Dkt.Tatenda Annastacia Mavetera amesema kwamba Tanzania na Zimbabwe zipo katika Mpango wa kushirikiana katika nyanja ya Mawasiliano ya Tehama na hivi karibuni wataingia Makubaliano hayo kuwezesha huduma za Posta katika nchi hizo.
Amesema kwamba yapo mambo yanayoathiri kwa Njia chanya utoaji wa huduma za Posta sio tu Tanzania hata barani Afrika na Duniani kwa ujumla Sasa Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia maanake yanatulazimisha sisi kuwekaza katika mkondo huo tusipofanya hivvyo umuhimu na huduma za mashirika ya Posta utaonekana umepitwa na wakati.
Kwa Upande wa Postamasta Mkuu Maharage Chande amesema kwamba amesema Sekta ya Posta inabadilika sana matumizi ya barua yamepungua na Kwa vijana hata Posta hawafiki kuleta barua tumezungumza hayo lakini tumeonyesha nini tunafanya kwenda na mbadiliko hayo na mipango ya Shirika letu.
Alisema kwa kifupi mtaanza kuviona kutoka Posta kwanza ni kutumia Teknolojia kuleta tija kwa wananchi na wateja kwa Shirika kwa kuongeza Duka Mtandao tunataka mama aliyepo Babati akitengeneza chungu akiweke katika Duka Mtandao na kuuza popote Ulimwenguni.
“Haya ndio Mageuzi ya sekta ya Posta tunayoyahitaji kuendana na mabadiliko ya Teknolojia ya Mawasiliano kupitia Shirika la Posta na tutakuwa na majengo ambayo yanaitwa vituo vya kuweka bidhaa zako ili watu waweze kununua kote Duniani tunataka Mtalii anaponunua bidhaa hana haja ya kukibeba kuzunguka nacho tunataka akutane nacho Australia”