Na. WAF – Dar es Salaam
Vifo vya watoto wa umri chini ya miaka Mitano vimepungua kutoka vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2016 mpaka vifo 43 kwa kila vizazi hai 1,000 2022.
Waziri Ummy amesema hayo Januari 10, 2024 wakati akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za Afya nchini kwa mwaka 2023 wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es salaam.
Pia, Waziri Ummy amesema vyumba vya uangalizi maalumu vinavyohudumia watoto wachanga walio mahututi (Neo natal Care units) vimeongezeka kutoka Hospitali 125 mwaka 2022 hadi Hospitali 189 mwaka 2023.
“Tukirudi nyuma kidogo kwa mwaka 2018, Tanzania ilikuwa na NICU 14 tu na hii ina maana nchi ilikuwa na ombwe kubwa la huduma za Afya kwa watoto wachanga na hivyo watoto wengi kufariki kwa kukosa huduma stahiki.” Amesema Waziri Ummy