Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui Kampuni ya StarTimes nchini Tanzania Bw. David Malisa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 16, 2024 Jijini Dar es Salaam kuhusu fainali za msimu wa 14 za Bongo Star Search (BSS) zinatarajiwa kufanyika Januari 27, 2024 kuanzia saa 12:00 jioni katika ukumbi wa Warehouse Masaki, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Production na Mwanjilishi wa BSS Madam Rita Paulsen akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 16, 2024 kuhusu fainali za msimu wa 14 za Bongo Star Search (BSS) zinazotarajiwa kufanyika Januari 27, 2024 kuanzia saa 12:00 jioni katika ukumbi wa Warehouse Masaki, Dar es Salaam.
Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Agustino Makame akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 16, 2024 kuhusu fainali za msimu wa 14 za Bongo Star Search (BSS) zinazotarajiwa kufanyika Januari 27, 2024 kuanzia saa 12:00 jioni katika ukumbi wa Warehouse Masaki, Dar es Salaam.
Meneja wa Kampuni ya kuuza Viwanja EPL Bw. Athumani Magembe akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 16, 2024 kuhusu fainali za msimu wa 14 za Bongo Star Search (BSS) zinazotarajiwa kufanyika Januari 27, 2024 kuanzia saa 12:00 jioni katika ukumbi wa Warehouse Masaki, Dar es Salaam.
………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Fainali za msimu wa 14 za Bongo Star Search (BSS) zinatarajiwa kufanyika Januari 27, 2024 kuanzia saa 12:00 jioni katika ukumbi wa Warehouse Masaki Jijini Dar es Salaam, huku mshindi wa kwanza anatarajia kupata zawadi ya shillingi milioni 20 pamoja na kiwanja.
Katika fainali hizo za msimu 14 za BSS watanzania watashuudia mubashara katika channel ST Swahili kupitia king’amuzi cha StarTimes, huku wadau mbalimbali hasa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakitakiwa kununua tiketi za kuingilia ambazo zinapatikana katika maeneo mbalimbali ikiwemo maduka yote ya StarTimes, kitaambaa cheupe Sinza, Palm Village Mikocheni pamoja na Wherehouse Masaki.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 16/1/2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Production na Mwanjilishi wa BSS Madam Rita Paulsen, amesema kuwa mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto kutoka na washiriki wengi kuwa na vipaji.
Madam Rita amesema kuwa Mikoa mbalimbali wamepata fursa ya kushiriki katika mashindano hayo ambapo Mkoa wapata washiriki sita badala ya watano kutoka na uwepo na idadi kubwa ya vijana wenye vipaji.
“Tulitakiwa kila mkoa tuchukue watu watano lakini kuna mikoa tulilazimika kuchukua idadi ya zaidi ya watano lengo ni kuwapa nafasi waonekane na wasonge mbele” amesema Madam Rita.
Amefafanua kuwa mshindi wa kwanza atapata shilingi 20 pamoja na kiwanja cha kujengea nyumba, huku akitoa fursa kwa wadau kutoa zawadi kwa mshiriki anayempenda.
Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui Kampuni ya StarTimes nchini Tanzania Bw. David Malisa, amesema kuwa kila msimu BSS imekuwa ikipiga hatua kwa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Bw. Malisa amesema kuwa lengo ni kuwafikia watanzania wengi ili waweze kuonesha vipaji vyao na kufikia ndoto zao.
Amesema wakati umefika kwa wakazi wa Dar es Salaam kushiriki katika fainali za BSS, huku akitoa fursa kwa wakazi kutoka mikoani mbalimbali kufatilia fainali hizo kupitia channel ST Swahili katika king’amuzi cha StarTimes.
“Wakati umefika wa kujiunga na familia ya StarTimes ili kuweza kupata burudani na kutazama vipaji kwa bei ya punguzo kwa sh 25,000 hadi sh 56,000” amesema
Bw. Malisa.
Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutazama ST Swahili ili kujua nani na nani wameweza kuingia katika nafasi sita za juu katika kuwania nafsi ya kwanza katika mashindano ya BSS.
Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Agustino Makame, amesema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha malengo yanafikiwa katika kukuza vijapi vyao vijana kwa ajili ya kujipatia kipato.