Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komredi Kheri James mapema leo amefanya ziara ya kikazi katika shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri mbili za wilaya ya Mbulu, kwa lengo la kuendelea Kufuatilia zoezi la kupokea Wanafunzi pamoja na mwenendo wa masomo.
Akizungumza katika ziara hiyo Komredi Kheri James amewapongeza Wakurugenzi na wakuu wa shule kwa kusimamia vyema zoezi la kupokea Wanafunzi, na kuwataka kuhakikisha ratiba za masomo zinaendelea kwa Wanafunzi ambao tayari wamewasili shuleni.
Kheri James ametumia fursa hiyo pia kuwaeleza wakuu wa shule kuwa ni marufuku kumrudisha mtoto nyumbani kwa sababu ya mchango, au mashariti mengine yoyote ambayo yanapingana na miongozo ya elimu nchini.
Aidha Kheri James amewahimiza wazazi, viongozi na Wananchi wote kuhakikisha kuwa kila mtoto anaestahili kuwa shule ana fikishwa shuleni.
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Mkuu wa wilaya aliambatana na Wakurugenzi wa Halmashauri Mbili za wilaya ya Mbulu, Maafisa Elimu pamoja na maafisa waandamizi wa idara ya elimu.
Wilaya ya Mbulu inaendelea Kufuatilia na kusimamia kwa ukaribu zoezi la kupokea wanafunzi katika shule zote ili kuhakikisha kuwa lengo la Serikali la watoto kupata elimu linafanikiwa vizuri na kwa ufanisi.