Katibu mtendaji baraza la usimamizi wa leseni Hawah Ibrahim Mbaye akitoa maelezo katika maadhimisho ya siku ya leseni yaliyofanyika Ukumbi wa Dkt. Hussein Mwinyi kituo cha maonesho ya Biashara nyamazi Zanzibar .
Katibu mkuu wizara ya biashara na maendeleo ya Viwanda Ali Khamis Juma akimkaribisha waziri wa Wizara hiyo Omar Said Shaaban kuhutubia katika maadhimisho ya siku ya leseni yaliyofanyika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi kituo cha maonesho ya Biashara nyamazi Zanzibar.
Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda Omar said Shaaban akihutubia katika maadhimisho ya siku ya leseni yaliyofanyika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi kituo cha maonesho ya Biashara nyamazi Zanzibar.
Waziri wa biashara na maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban akimkabidhi cheti cha shukuani aliekuwa Waziri wa biashara na Viwanda balozi Amina Salim Ali katika maadhimisho ya siku ya lesesni yaliofanyika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi kituo cha maonesho ya Biashara nyamazi Zanzibar.
Waziri wa biashara na maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban akimkabidhi cheti cha shukuani katibu mkuu wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia ,wazee na watoto Abeda Rashid Abdalla katika maadhimisho ya siku ya lesesni yaliofanyika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi kituo cha maonesho ya Biashara nyamazi Zanzibar.
Wasanii wa maigizo kikundi cha Kirobo Art Group wakifanya igizo lenye mnasaba wa umuhimu wa kukata leseni maadhimisho ya siku ya lesesni yaliofanyika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi kituo cha maonesho ya Biashara nyamazi Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia maadhimisho ya siku ya lesesni yaliofanyika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi huko kituo cha maonesho ya Biashara Nyamazi Zanzibar.
………………………..
Na Rahma Khamis Maelezo 15/1/2024
Waziri wa Biashara na msaendeleo ya viwanda na Mhe Omar Said Shaban amezitaka mamlaka zinazohusika na utoaji wa leseni s kutojihusha na vitendo vya rushwa ili kuondoa urasimu.
Wito huo ameutoa katika Ukumbi wa Dkt Mwinyi Nyamanzi Wilaya ya Magharib B’ katika maadhimisho ya siku ya leseni ikiwa ni kusherehekea miaka 60 ya mapinduzi.
Amesema kuwa rushwa ni jambo ambalo linarejesha nyuma upatikanaji wa haki katika utoaji wa huduma hivyo ni vyema kutojihusisha na vitendo hivyo ili kufikia malengo.
Ameeleza kuwa siku hiyo ni muhimu kwani inatoa fursa kwa mamlaka husika na watumiaji wa leseni kutambua wajibu wao katika kazi.
Aidha amefahamisha kuwa Kauli mbiu ya maadhimsho hayo inaakisi upatikanaji wa haki na itakua chachu ya maendeleo kwa wafanyabiashara na Wizara kuhakikisha biashara zinakua na kuinua pato la taifa.
Amesesema Serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Dkt Mwinyi inaendelea kuhakikisha wananchi na wafanyabiashara wànapata huduma bora kila siku.
Ameongeza kwa kusema kuwa endapo mamlaka ya leseni itatekeleza kazi zake ipasavyo itaondosha urasimu kwa watumiaji wa leseni.
“Utoaji wa leseni isiwe chanzo cha kuingiza kipato kwani kuna baadhi ya Mamlaka zinajipatia kipato kwa kuongeza kipato kila mwaka jambo ambalo no kosa kisheria, alifahamisha Waziri Shaaban.
Aidha amezitaka Mamlaka husika kutambua haki na wajibu ili kuhakikisha wateja wanaowahudumia wanafahamu haki na wajibu wao katika maombi ya kukata leseni.
Hata hivyo amezikumbusha Mamlaka husika kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili watambue huduma zinazotolewa na mamlaka hizo.
” Kuna wafanyabiashara wanafanya biashara zao bila ya kufahamu huduma muhimu zinazotolewa katika Mamlaka husika”alisema Waziri.
Akitoa salamu za Wizara Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ali Khmis Juma amesema kuwa baraza lina kazi kubwa ya kuwadhibiti watoaji na watumiaji wa leseni ili kuondoa makalamiko.
Nae Katibu Mtendaji Baraza la Usimamizi wa Leseni Hawah Ibrahim Mbaye amefahamisha kuwa baraza limefanikiwa kupunguza utitiri wa leseni zilizokua zikitolewa bila kuzingatia muongozo .
Ameongeza kuwa baraza linaendelea kusisitiza wafanyabiashara kukata leseni ili kuongeza pato la taifa na kuwaweka huru na salama wakati wakifanya bishara zao.
Aidha amesema kuwa baraza linafanyakazi kupitia majadiliano ili kukuza uchumi na kufikia malengo.
Kwa mara ya kwanza Baraza la Usimamizi wa Leseni Zanzibar limeadhimisha siku ya leseni ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Leseni bila Uarasimu inawezekana.”