Timu ya Taifa ya Ivory Coast imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Guinea-Bissau katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Mataifa ya Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara nchini humo.
Mabao ya Timu ya Taifa ya Ivory Coast yalifungwa na Seko Fofana Dakika ya 4 pamoja na Jean-Philippe Krasso dakika ya 58 ambayo yalitosha kabisa kuipa ushindi mwenyeji wa michuano hiyo.
Kufatia matokea hayo Ivory Coast inaongoza kundi A baada ya kukusanya pointi tatu.