Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura, jana 12 Januari 2024 ameshiriki pamoja na waombolezaji wengine kwenye mazishi ya aliyekuwa Naibu Kamishna wa Polisi Mstaafu DCP Eliah Magwe Kehengu.
Marehemu DCP Magwe lifariki Dunia tarehe 06 Januari 2024 katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu na mazishi yake yamefanyika tarehe 12 Januari 2024 Mugumu, Serengeti Mkoani Mara.