Mkurugenzi wa Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Condrad Millinga akizungumza wakati wa kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Tarehe 11 Januari 2024. Aliyekaa ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mhe. Janeth Mayanja.
baadhi ya wafanyabiashara Wilayani Hanang’ katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara Tarehe 11 Januari 2024.
Mwenyekiti wa Soko la Hanang’ Bw. Mathia Jonisi akizungumza katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Mnyara Tarehe 11 Januari 2024.
Wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Tarehe 11 Januari 2024.
Bw. Godfrey Chacha Afisa Vijana Mwandamzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Tarehe 11 Januari 2024.
NA; MWANDISHI WETU HANANG’
Taasisi za kifedha Hususani Mabenki, yameshauriwa kuja na Dirisha maalum na Products zitakazosaidia wafanyabiasha wadogo walioathiriwa na maafa ya maporomoko ya tope, miti na mawe yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana Wilayani Hanang’ Mkoa wa Manyara.
Hayo yamesemwa tarehe 11 Januari 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Bi Janeth Mayanja alipokutana na Wafanyabiashara wilaya hiyo na wawakilishi wa mabenki na Taasisi za kifedha katika Mkutano wa Mafunzo Ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC).
Bi. Mayanja alisema ni wakati sasa kwa mabenki kuwafikiria wafanyabiashara wadogo wasiyo na mali ya kuweka rehani katika kupata mikopo yenye unafuu kuja na Products zitakazowawezesha wafanyabiasha hao kukopesheka kwa riba nafuu kwani wafanyabiashara hao wanakopa kwenye taasisi nyigine za kifedha zenye masharti magumu na kwa watu binafsi na wanaweza kulipa.
“Inawezekana mikopo hivyo kwa mabenki ikaonekana ni midogo midogo kwa sababu wafanyabiahara hao ni wengi lakini bado mabenki yanaweza kupata faida, tukiendelea kijikita kwa wafanyabiashara wakubwa wenye mali za kuweka rehani maendeleo ya watanzania wanaojikita kwenye biashara ndogondogo yatachelewa.” Alisema Mhe. Mayanja
Kwa wakati huo huo Banki ya NMB imekabidhi hundi ya fedha ya Tsh 269,000,000 (Milioni Mia Mbili sitini na tisa) kwa Waathirika kumi na nane wa maporomoko ya Mlima Hanang , ambapo fedha hizo ni sehemu ya fidia kwa wateja wa Benki hiyo waliokata Bima kwenye Biashara na Bima za Mikopo Kupitia Bank ya NMB, na imeelezwa kuwa Benki hiyo itaendelea kutoa Elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa Bima.
Awali Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo Wilayani Hanang’ kuchangamkia fursa zitakazotolewa na mabenki hayo na kuachana na mikopo yenye masharti kandamizi ili kuwainua kiuchumi