Na Sophia Kingimali.
Baraza la Mitihani la Taifa limetangaza rasmi matokeo ya kidato cha pili na darasa nne ambapo umekuwa na ongezeko kubwa la ufaulu huku wanawake wakiongoza kwa ufaulu kwa asilimia 6.
akizungumza wakati akitangaza matokeo hayo leo januari 7,2024 katibu mtendaji wa NECTA Dkt. Said Mohamed amesema matokeo hayo yamechangiwa na utulivu na kuzingatika taratibu za mitihani pamoja na mafunzo waliyoyapata wanafuzi.
“Kati ya wanafunzi waliofaulu kuendelea na darasa la tano wasichana 681,259 sawa na asilimia 84.79 na wavulana ni 606,675 sawa na asilimia 81.78 takwimu zinaonyesha kuwa wasichana wamefaulu vizuri ikilinganishwa na wavulana huku kidato cha pili wasichana 405,878 sawa na asilimia 53.42 na wavulana 353,921 sawa na asilimia 46.58″amesema Mohamed
Amesema ufaulu wa masomo ya hisabati na sayansi na teknoliojia kwa darasa la nne umepanda kwa asilimia 4.30 ikilinganishwa na mwaka 2022.
Amesema katika somo la sayansi na Teknoloji wasichana wamefaulu vizuri kuliko wavulana kwa asilimia 1.63 na huku somo la hisabati wakiongoza wavulana.
Sambamba hayo baraza limefuta matokeo yote ya wanafunzi waliofanya udanganyifu pamoja na kuandika lugha za matusi kwenye mitihani yao.
“178 waliofanya udanganyifu na watatu walioandika matusi kwenye scripti zao katika upimaji wa kitaifa wa darasa la nne huku kidato cha pili waliofanya udanganyifu wakiwa 28 na walioandika matusi wakiwa 14″amesem Mohamed.
Akizungumzia ufaulu wa jumla kwa kidato cha pili amesema jumla ya wanafunzi 592,741 kati ya 694,769 wenye matokeo ambao sawa na asilimia 85.31 wamefaulu ambao wamepata madaraja 1 mpaka 4.