RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kuunga mkono ajenda ya maendeleo endelevu Visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Akizungumza mara baada ya kushiriki katika matembezi ya sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar yaliyofanyika Zanzibar Mjini, Dkt Mwinyi aliipongeza benki hiyo huku alibainisha kuwa msaada wa Benki ya NMB umekuwa chachu katika kukuza uchumi, na kuleta maendeleo endelevu Visiwani humo.
“Benki ya NMB imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Serikali yetu katika kuchochea maendeleo ya sekta mbalimbali za Zanzibar. Natumia fursa hii kuipongeza benki ya NMB kwa kuendelea kutuunga mkono na ningependa kuchukua fursa hii kuyaomba mashirika wengine yanayofanya kazi Visiwani hapa kuunga mkono ajenda yetu ya maendeleo,” amesisitiza Rais Mwinyi.
Awali, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Tabia Maulid Mwita naye aliimwagia sifa benki hiyo na kuongeza kuwa benki hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kukukuza maendeleo ya sekta ya michezo Visiwani Zanzibar.
Mwita alishukuru benki hiyo kwa kushiriki kikamilifu katika matembezi ya sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar baada ya benki hiyo kutoa udhamini wa shilingi milioni 200 wa vifaa vya michezo hivi karibuni.
Alisisitiza dhamira ya Wizara ya kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa Zanzibar ili kuimarisha maendeleo ya michezo.
Naye Meneja wa Bashara ya Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Said Shaame wakati wa hafla hiyo alisisitiza dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuongeza kuwa benki hiyo mbali na kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo imekuwa na mchango mkubwa katika kuwekeza katika uwekezaji wa kijamii wa kijamii (CSIs) ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kukuza thamani ya wadau wake wote ikiwa ni pamoja na jamii ambako benki inafanyia kazi.
“Sisi kama benki, tutaendelea kuunga mkono kikamilifu utekelezaji wa Ajenda ya Uchumi wa Bluu ya Serikali ya Zanzibar kupitia utoaji wa huduma bora za kibenki ninazokidhi matakwa ya wateja wetu,” alisema.