NA VICTOR MASANGU,KISARAWE
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Dkt.Seleman Jafo amewataka viongozi na watendaji kujikita zaidi katika kusimamia na kukamilisha ipasavyo miradi mbali mbali ya maendeleo lengo ikiwa ni kuwahudumia wananchi.
Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutembelea miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi ili kubaini changamoto zinazowakabili.
Waziri Jafo katika ziara hiyo ameweza kupata fursa ya kuwatembelea na kuzungumza na wananchi wa maeneo ya vijiji katika Kata za Marui,Vikumburu pamoja na Chole na kuwahakikishia kuwaboreshea huduma za kijamii kama vile maji safi na salama,afya elimu na mambo mengi ya msingi.
Jafo alibainisha kwamba lengo lake kubwa katika Amesema katika jimbo hilo ni kuweka mikakati ya kila kijiji kuwa na zahanati ifikapo mwaka 2025 ili kuwaondolea adha wananchi ya kutembea umbari mrefu ya kufuata huduma ya maji.
Alisema endapo miradi inayopelekwa kwa wananchi viongzi wataisimamia kama ilivyopangwa itaondoa vikwazo kwa jamii na wataendelea na shughuli nyingi e za maendeleo kuinua uchumi wao.
Katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa Zahanati ngazi ya Vijiji zaidi ya milionin 50 zimetolewa kutoka mfuko wa Jimbo kujenga miradi hiyo na kwamba ifikapo Machi mwaka huu zipo ambazo zitaanza kutoa huduma.
“Nimetembelea miradi ya nyumba ya mwalimu Ngongere shule ya Msingi na nimeelekeza kupitia fedha za mfuko wa jimbo ikamilike kwa wakati hawa walimu wapate sehemu ya kuishi” alisema.
Kadhalika alisema wataalamu wanatakiwa kubadilika na kuzingatia fedha zinazotengwa zinafika kwa wakati maeneo ya miradi ili wanufaika waondokane na vikwazo .
Katika hatua nyingine Waziri Jafo alipongeza mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Mafumbi iliyopo kata ya Chole ambapo alisema uongozi wa Kijiji hicho unatakiwa kuigwa kutokana na usimamizi mzuri wa fedha wanazopatiwa.