NJOMBE
Katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe Josaya Luoga amesema kwamba chama kinaendelea kuwa bora na kutazamwa kwa ukaribu na vyama vingine Duniani kutokana sababu mbambali ikiwemo kuongoza kwa muda mrefu,namana ya upatikanaji wa viongozi wake pamoja na kushinda kwenye chaguzi.
Luoga ameeleza hayo wakati akizungumza na viongozi kwenye mkutano wa halmashauri kuu ya Chama hicho ngazi ya kata kwenye kata ya Lubonde wilayani Lubonde akitaka viongozi kuendelea kushirikiana kuimarisha Chama hicho ili waweze kuendelea kushika dola.
“Chama cha Mapinduzi ni Chama bora namba mbili duniani baada ya Chama cha CPC cha China na hii ni kwasababu ya mfumo wa uongozi,utaratibu wake wa upatikanaji wa uongozi na namna tunavyoshinda uchaguzi,lakini ndio Chama namba moja Duniani kinachoendelea kuongoza taifa kwenye mataifa yenye mfumo wa vyama vingi kwa hiyo Tanzania ndio nchi pekee ambayo ina Chama tawala toka nchi iingie kwenye mfumo wa vyama vingi”amesema Luoga
Awali diwani wa kata ya Lubonde Ediga Mtitu ameomba Chama cha Mapinduzi kuwa na imani na viongozi ndani ya kata hiyo kwa kuwa wameendelea kushirikiana siku zote kwenye utekelezaji wa miradi inayoendelea licha kuwepo kwa vikundi vya watu wachache ambao wanajaribu kufifisha jitihada za wengi.
“Lazima tuendelee kushirikiana ili tuhakikishe yale mambo ambayo tunatamani yawe basi yanakuwa na sio kwa maamuzi yangu mimi ila ni maamuzi ya pamoja”Amesema Mtitu
Kwa upande wake mtendaji wa kata ya Lubonde Anna Mwalongo amesema kutokana na ushirikiano uliopo baina yao na viongozi wa ngazi za juu akiwemo Mbunge na diwani wameweza kupata miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa kwenye idara ya afya,elimu,maendeleo ya jamii kilimo pamoja na ufugaji huku akiishukuru serikali kwa kutoa fedha kutekeleza miradi mingi katika eneo Hilo.