Kamanda Mallya akiwa ameambatana na watoto wawili ambao aliwahi kukutana nao wakati akitoa elimu ya ushirikishwaji jamii kwa makundi mbalimbali, watoto hao ni Samwel Patrick Ndolimana kutoka Shule ya Msingi Juhudi na Ivanka Klif Nzunda kutoka Shule ya Msingi Haloli wote ni wanafunzi wa darasa la Pili katika shule hizo, kitendo hicho kilimpelekea kuwakutanisha watoto hao na watoto wenzao katika tukio hilo ili waweze kufurahia kwa pamoja.
Akizungumza na wazazi/walezi pamoja na watoto hao alisema “Ulinzi wa kuwalinda watoto na wanafunzi unaanza na sisi tuwe makini sana kipindi hiki cha mwishoni mwa mwaka kwani watoto wengi upotea na hufanyiwa ukatili hivyo basi mzazi/mlezi unatakiwa kumlinda mtoto wako kama mboni ya jicho lako au simu yako ili kumuepusha na vitendo hivyo anapokuwa njiani, mtaani na nyumbani kwa kufanya hivyo kutawaweka watoto wetu salama” alisema Kamanda Mallya.
Naye Mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Rita Kamenya alimshukuru kwa dhati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe kwa kushiriki katika tukio hilo na alitumia fursa hiyo kumkabidhi zawadi ya keki kuonesha ishara ya upendo na baada ya kupewa keki hiyo aliamua kuifungua na kuwagawia watoto ambao waliohudhuria katika tukio hilo ili kuendelea kujenga na kuimarisha uhusiano na urafiki pia alitumia fursa hiyo kwa kula pamoja.
Sambamba na hilo, Kamanda Mallya aliwasisitiza kutosita kutoa taarifa mbalimbali za uhalifu ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya yao.