Katibu Mkuu Ofisi ya raisi tawala za mikoa Serikali za mitaa na idara maalum za SMZ Issa Mahfoudh Haji akininua chaza wakati wa uzinduzi wa soko la mazao ya baharini uliyofanyika Kikungwi Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi..
Mkuu wa Wilaya ya Kati Sadifa Juma khamis akininua chaza wakati wa uzinduzi wa soko la mazao ya baharini uliyofanyika Kikungwi Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi.
Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja Mhe.Ayoub Muhammed Mahmoud akininua chaza wakati wa uzinduzi wa soko la mazao ya baharini uliyofanyika Kikungwi Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi..
Baadhi ya wajasiriamali wakifurahia uzinduzi wa soko la mazao ya bahari uliyofanyika Kikungwi Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa soko la mazao ya bahari liliopo kikungwi Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi..
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui akikata utepe kuashiria uzinduzi wa soko la mazao ya bahari liliopo kikungwi Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui akiwa na Mwakilishi wa Jimbo la tunguu Simai Muhammed Said ,mkuu WA mkoa wa Kusini Unguja wakipata maelezo kuhusiana na wajasiriamali wa eneo hilo kutoka kwa Nahodha wa vyombo vya utalii na uvuvi wa chaza bahati Issa Sleiman wakati wa uzinduzi wa soko la mazao ya bahari liliopo kikungwi Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi..
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui akipata maelezo kuhusiana na ujenzi wa soko la mazao ya bahari kutoka kwa Msimamizi wa mradi kutoka Kampuni ya modern building contractor Ltd Ali Pandu Sharifu wakati wa uzinduzi wa soko Hilo huko Kikungwi Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi. PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
………
NA ALI ISSA MAELEZO
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amewataka wajasiriamali wa Soko la Chaza Kikungwi kudumisha usafi ili liwe endelevu na kivutio kwa Watalii.
Akizungumza katika uzinduzi wa Soko la mazao ya baharini, huko Kikungwi Wilaya ya Kati, ikiwa ni shamrashamra ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema Watalii wanaoingia nchini wanapenda mazao ya Baarini ikiwemo Chaza hivyo ni vyema kudumisha usafi katika maeneo yao.
” Usafi ni muhimu na biashara ya Chaza inapendwa na wageni wa kitalii” alisema Waziri.
Aidha amewataka kufuata utaratibu wa wafanyabiashara wa chakula kwa kupima Afya zao na kuvaa nguo maluum zinazotakiwa.
Akisoma taarifa ya kitaalamu, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Malum za SMZ Issa Mahfoudhi Haji alisema ujenzi wa Soko hilo itapelekea kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao.
Nae Katibu wa kikundi Cha kuuza Chaza Kikungwi Bahati Issa Suleiman alisema kuwepo kwa Soko hilo kumewapa faraja kwani ni Soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao sambamba na kuahidi kulienzi na kulitunza ili liweze kuwa endelevu.
Soko hilo limejengwa na kampuni ya Mzawa Modarn Building Contractor LTD, umegharimu zaidi ya milioni 300 ambapo ujenzi wake ulianza tarehe 23/3/2023 na umekamilika rasmi 25/11/2023.